Maofisa wa Jeshi wakiwa wamekaa kuangalia maonesho mbali mbali yaliyokuwa yakiendelea uwanjani |
Vijana wa Jeshi wakiwa katika Gwalide |
Baadhi ya wananchi wakiwa wanaonyesha maandamo makali, ambapo kikosi cha jeshi kilikwenda kutuliza fujo hizo (picha za chini utaona walivyojeruhiwa na kubebwa machela. |
Raia amebebwa machela baada
ya kupatiwa kipondo toka kwa wanajeshi wakati walipokatazwa kuandamana
nao wakiwa wanaendelea na maandamoano yao.
|
JESHI LA WANANCHI limesema kwa sasa linakabilina na
changamoto ya kupambana na adui wa Ughaidi na si wale maadui wa kuwasubilia
mipakani kama ilivyokuwa kipindi cha miaka ya nyuma.
Hayo yalisema na Mkuu wa chuo cha mafunzo ya huduma na
Utawala cha Kijeshi , Luten Kanali Machera Machera , wakati wa maadhimisho ya
miaka 48 ya Jeshi la Wananchi tangu kuanzishwa yaliyofanyika Mjini Morogoro
katika viwanja vya chuo hicho.
Alisema Jeshi linazidisha umakini zaidi katika kutoa mafunzo
mbalimbali ili kukabiliana na changamoto zilizopo za ughaidi hapa nchi.
Kanali Machera Machera, alisema miaka ya nyuma jeshi
lilikuwa likipambana na maadui wa mipakani ambao wanatoka nchi nyingine na
kuvamia, lakini kipindi hiki adui anatoka ndani na si nje kama ilivyokuwa
ikidhaniwa.
“Sasa adui yupo ndani kwani vitendo vya ughaidi vinafanywa
hapahapa ndani , hali ambayo ni hatali kwani huwezi kutambua haraka pale
anapotokea sasa jeshi lipo imara sana na
litaendelea kutoa mafunzo ili kujiimarisha zaidi”Alisema Kanali Machera.
Aidha katika maadhimisho hayo jeshi lilifanya huduma za
kijamii kama kufanya usafi katika kituo cha afya zahanati iliyopo Kinguruila, kutembelea
hospitali ya mkoa na kutoa mchango wa damu na
kuwaona wagonjwa na kufanya usafi katika soko la Manspaa hiyo .
Pia michezo mbalimbali ya kijeshi ilioneshwa kama Gwaride,
mpira wa miguu, mpira wa nyavu,kukumbiza kuku na kutuliza fujo za maandamo.
No comments:
Post a Comment