TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, September 26, 2012

REDDS MISS TANZANIA 2012 KUFANYIKA NOV 03 UBUNGO PLAZA



Salha Israel (kulia) akifurahia zawadi yake ya gari aina ya Jeep wakati akikabidhiwa mwaka jana chini ya wadhamini wa waliopita kampuni ya huduma za simu ya Vodacom. Shindano hilo sasa linadhaminiwa na bia ya Redds.

Salha Israel (wa pili kushoto) akifurahia zawadi yake ya gari aina ya Jeep wakati akikabidhiwa mwaka jana chini ya wadhamini wa waliopita kampuni ya huduma za simu ya Vodacom. Shindano hilo sasa linadhaminiwa na bia ya Redds.

Salha Israel akiwa katika bango la Redds Miss Tanzania 2012 wakati wa uzinduzi wa shindano la mwaka huu


SHINDANO la Redds Miss Tanzania 2012 litafanyika Novemba 3 kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, waandaaji kamati wa Miss Tanzania wametangaza leo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam, mratibu wa shindano hilo, Hashim Lundenga, amesema warembo wataingia kambini Oktoba 2 katika hoteli ya Giraffe, ambako watakaa hadi siku ya shindano.
  
Mshindi wa shindano hilo atamrithi, Salha Israel kutoka Ilala anayeshikilia taji la taifa. Kwa kushinda shindano hilo mwaka jana, Salha alizawadiwa gari kali aina ya Jeep.

Hata hivyo, mapema mwaka huu kamati hiyo iliendesha shindano dogo na kumpata Lissa Jensen ambaye aliwakilisha nchi katika fainali za Dunia kutokana na mabadiliko ya kalenda yaliyofanywa na Kamati ya Miss World.

Miss Tanzania atakayepatikana Novemba 3 atakuwa na muda mrefu wa kujiandaa na atashiriki katika shindano la Miss World la mwakani na utaratibu huo utakuwa wa kudumu.

Hadi sasa, Miss Tanzania aliyepata mafanikio katika shindano hilo la dunia ni Nancy Sumary ambaye alitwaa taji la Miss World Africa 2005.

No comments:

Post a Comment