TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, September 30, 2012

KASHFA NYINGINE YAIBUKA TANESCO
 Na:Fidelis Butahe,Mwananchi

KASHFA mpya imeibuka ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), baada ya kubainika kuwa vikombe vya kufungia nyaya za umeme vyenye thamani ya mamilioni ya fedha vimetelekezwa kutokana na baadhi ya vigogo wa shirika hilo kushindwa kunufaika na mradi huo.

 Habari kutoka ndani ya shirika hilo zinaeleza kuwa vigogo hao wanadaiwa kuvikataa vikombe hivyo kwa maelezo kuwa ni vibovu, baada ya mzabuni kushindwa kuwaona vigogo hao. Wakati vigogo hao wakivikataa vikombe hivyo kwa madai kuwa ni vibovu, taarifa zinaeleza kuwa wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamethibitisha kuwa vikombe hivyo ni vizuri na havina matatizo yoyote. Hatua ya Tanesco kupeleka vikombe hivyo kuthibitishwa na wataalamu wa Chuo Kikuu, Kitengo cha Uhandisi ilitokana na mvutano uliokuwapo baada ya vigogo walioshindwa kunufaika na mradi huo kutoa maelezo kuwa vikombe hivyo havina viwango bora. 

Hata hivyo, uchunguzi unaonyesha kuwa licha ya vigogo hao kuvikataa vikombe hivyo zaidi ya 40,000 vyenye thamani ya Sh900 milioni kwa madai kuwa vibovu, tayari shirika hilo limekuwa likivitumia katika nguzo zake zenye umeme mkubwa kwa miaka mingi. Mvutano wa viongozi hao ndani ya shirika hilo, umesababisha mradi wa kukarabati njia za umeme mkubwa bila ya kuzima umeme kwa kuondoa vikombe vilivyochakaa uliokuwa ukifanyika katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kusimamishwa mapema mwaka huu. 

Baadhi ya wataalamu wa Tanesco wanaeleza kuwa vikombe hivyo kama vitatumika vina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya kufunga vikombe vipya katika njia ya umeme mkubwa wa kutoka kwenye mtambo wa kuzalishia umeme wa Kidatu mkoani Morogoro hadi Ubungo jijini Dar es Salaam. Pia, kumalizia ukarabati wa njia ya umeme ya Arusha hadi Moshi mkoani Kilimanjaro iliyositishwa. 

Chanzo chetu kutoka ndani ya Tanesco kinaeleza kuwa vikombe vilivyopo katika njia ya umeme ya Kidatu hadi Ubungo havijabadilishwa kwa miaka mingi hali ambayo inafanya umeme kupotea njiani kwa asilimia nyingi. Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Tanesco, Felschami Mramba alisema kuwa mikataba ndani ya shirika hilo ni mingi na kusisitiza kuwa hawezi kulijibu suala hilo mpaka atakapowasiliana na kitengo cha ununuzi cha shirika hilo. 

“Kwa sasa sina maelezo ya kina ya mikataba, hasa kuhusu suala hilo unaloniuliza, lakini mpaka wiki ijayo nitakuwa nimefuatilia na kupata jibu sahihi,” alisema Mramba. Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulika Nishati, George Simbachawene alisema suala hilo halijafika kwake.

 Simbachawene alisisitiza: “Mambo yanayofika katika ofisi yangu huwa kama malalamiko yanayoletwa na watu kutoka Tanesco na sehemu nyingine. Nikiyapata naanza kufuatilia ili kujua nini kinaendelea.” Alisema kuwa Tanesco ni shirika linalojitegemea katika utendaji wake wa kazi na ndiyo maana lina bodi yake, ambayo hukaa na kupanga mambo mbalimbali ya kufanya.

 “Wakati mwingine wizara inaingilia utendaji wa Tanesco kama tunaona kuna mambo hayaendi sawa, ila hili la ununuzi kwa kweli sijui kwa sababu halijafika ofisini kwangu kama lalamiko,” alisema Simbachawene na kushauri kuwa atafutwe Mramba. Hoja ya kuvikataa vikombe hivyo ambayo imekuwa ikitolewa na baadhi ya vigogo hao wa Tanesco ni kwamba vikombe hivyo ni vizito na nguzo haziwezi kuvibeba, vibovu na kwamba havifai katika ule utaratibu wa kufanya matengenezo bila kuzima umeme. Tanesco imekuwa ikikumbwa na kashfa mbalimbali zikiwamo matumizi mabaya ya fedha za shirika kwa baadhi ya maofisa kutumia zabuni kujinufaisha. Hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi William Mhando alisimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo.

 Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ilieleza kuwa Mhando alisimamishwa kazi pamoja na watendaji wakuu wengine wa Tanesco ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka. 

 Viongozi wengine wa Tanesco waliosimamishwa kazi ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi wa Ununuzi, Haruni Mattambo. 
Matatizo mengine ambayo yanadaiwa kuikumba Tanesco ni pamoja na uchakavu wa mitambo ya Tanesco, hujuma za miundombinu na kuingiwa kwa mikataba mibovu 
 Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari

Friday, September 28, 2012

BEREKING NYUUUZZZZ !!!:CCM YAIMWAGA CHADEMA KATIKA UMEYA JIJINI MWANZA

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekibwaga Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya mgombea wake wa kiti cha Umeya katika jiji hilo kujizolea kura 11 dhidi ya 8 ya mpinzani wake kwenye uchaguzi uliofanyika na kumalizika muda mfupi uliopita.
JK: AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA AFRICAN GREEN REVOLUTION MJINI ARUSHA

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo huku wajumbe wakiwa makini kumsikiliza.

Thursday, September 27, 2012

ZITTO: UBUNGE SASA BASI!
Zitto Kabwe


Na: Frank Sanga na Anthony Kayanda, Kigoma, MWANANCHI.

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais. Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma. Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.

 “Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi. “Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.

 “Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu. “Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.” Atangaza kugombea urais Katika hatua nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. “Kwanza nataka niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii,” Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea. 

Hata hivyo Zitto alipoulizwa baadaye na Mwananchi kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika katiba mpya.”

 “Nchi za Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi kama ilivyo katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo,” alisema Zitto Katika kukazia hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976 uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001, Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia 56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka 51 mpaka 46. Katika hatua nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila ila akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa. 

 “Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu,” alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.

 “CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?” Alihoji Zitto. Alisema ili kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania. 

 Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari
MAMBA MZITO ZAIDI MAREKANI ANASWA

Mamba aliyekamatwa Mississippi

MAMBA mwenye uzito wa kg. 316 amenaswa kufuatia juhudi ya kumsaka iliyofanywa na watu wanne kwenye ranchi ya Mississippi nchini Marekani na ameweka rekodi ya kuwa mamba mzito zaidi nchini humo.

Eneo la chini la Mississippi Delta linahusisha klabu nyingi za uwindaji, ardhi ya mbao, kilimo na maeneo ya hifadhi za wanyama.

Rekodi ya awali nchini humo ilikuwa ni mamba mwenye uzito wa kg. 312 na alikamatwa mwaka jana kwenye maji hayo hayo ya Delta.

Mamba huyo ana urefu wa futi 13 na inchi 1.5.

Hata hivyo, rekodi rasmi za mamba wakubwa zaidi duniani zinashikiliwa na mamba wawili wenye urefu wa futi 20 (mita 6.2) na kg 1,200.

Mamba wa kwanza aliuawa Mto Mary kaskazini mwa Australia mwaka 1974 na kupimwa na maafisa wa wanyama. Mamba wa pili aliuawa mwaka 1983 katika Mto Fly, Papua New Guinea. Katika suala la mamba wa pili, kilichopimwa kilikuwa ni ngozi ya mamba huyo na inafahamika kwamba ngozi pekee huwa inatoa vipimo pungufu vya urefu halisi wa mnyama, hivyo mambo huyo inawezkana alikuwa na urefu wa sentimeta 10 zaidi.
LEMA AFURAHIA KESI YAKE KUSIKILIZWA NA JAJI MKUU

Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Othman Chande
Godbless Lema
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa anaamini Mahakama ya Rufaa itapitia vyema vipengele vya kesi iliyompoka ubunge wake na kutoa uamuzi wa haki kwavile anamuamini Jaji Mkuu Mohamed Othman Chande.

Akizungumza katika mahojiano yake leo na kituo cha redio cha Clouds FM kupitia kipindi cha Bongo Amplifanya, Lema amesema kuwa yeye binafsi hataki kupendelewa bali haki itendeke na kwamba anaamini kuwa uamuzi wa jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa litakaloongozwa na Jaji Chande utakuwa ni wa haki na yuko tayari kuupokea.

"Sitaki upendeleo, nipendelewa nitaogopa, nitalia... niko tayari  kurudi kwenye uchaguzi, na ninaamini nitashinda kwa idadi ya kura za kubebwa kwenye canter.... nimefurahi kuwa kesi hii itaongozwa na Jaji Mkuu Chande," amesema.

'Yeye (Chande) ndiyo mkuu wa mahakama... ninaamini vipengele vitapitiwa kwa haki," amesema Lema ambaye ubunge wake ulitenguliwa na mahakama kutokana na kasoro kadhaa na hivyo akakata rufaa kupinga uamuzi huo

Wednesday, September 26, 2012

PRESIDENT KIKWETE MEETS KOFI ANNAN FOR AFRICAN GREEN REVOLUTION FORUM 1212 IN ARUSHA
The Chairman for Alliance for Green Revolution in Africa (AGRA) Kofi Annan land over to President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete his autobiograph titled "Intervetions, Alife in War and Piece" The book he CO Authored with Nader Mousavizadeh, Annan gave the President the book at Ngurdoto Mountain Lodge in Arusha shortly before the the opening of the Africa Green Revolution Forum yesterday evening . The main focus of the forum is scalling investiment and innovation for sustainable agricultural growth and food security
JK ANAYETAKA KUONDOKA CCM 'RUKSA'


NI WALE WANAOTISHIA BAADA YA KUTOSWA, AWASHANGAA WANAOTISHIANA SILAHA KWA AJILI YA UONGOZI

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amewatolea uvivu wagombea wa nafasi mbalimbali ambao majina yao yamekatwa, akisema wanaotaka kukihama chama hicho kwa sababu wametoswa, waondoke haraka. Licha ya kuwatakia safari njema, Rais Kikwete aliwatupia lawama baadhi ya wanaCCM ambao wameripotiwa kuendesha malumbano na kugeuza uchaguzi huo kama uwanja wa vita. Akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) jana, Rais Kikwete alisema kumekuwapo na taarifa mbalimbali ambazo zimemfikia pia kwamba baadhi ya wanachama wanatishia kukihama chama hicho kama majina yao yatakatwa.

 “Wako wenye ndimi mbili ambao wanasema kuwa wasipoteuliwa wanaweza kuondoka. Ah! Mimi nasema watangulie huko maana inaonyesha kuwa walishaandaa maeneo ya kwenda,” alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wajumbe wa Nec. Alisema CCM kinayo taarifa kuhusu watu kugombana na hata kutoleana silaha, jambo alilosema linashangaza, huku akihoji kuna nini katika uongozi tena Nec? “Uchaguzi usigeuzwe uwanja wa fujo. 

Wengine wanatoleana silaha kama majembe, ngumi na silaha nyingine, hivi wanagombana nini huko? Uchaguzi usigeuzwe kuwa ni uwanja wa vita.” alisema. Hivi karibuni, baadhi ya makada wa chama hicho wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali za kukitishia chama hicho akiwemo Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ambaye alikaririwa akisema kama jina lake halitapitishwa, patachimbika. Mbunge huyo alisema hayo siku chache baada ya jina lake kutupwa na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi iliyokuwa ikipitia na kuteua wagombea watatu kwa ajili ya kuwania nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya hiyo. 

"Hapatatosha CCM," alisema Mkono alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kutoswa kwake katika mchujo wa awamu hiyo ya awali. Ingawa Rais Kikwete hakutaja majina, Mbunge wa Nzega Dk Khamis Kigwangallah na Hussein Bashe nao waliripotiwa kutoleana maneno makali hata kuonyeshana bastola, huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja na Mbunge wa Kahama, James Lembeli wakiendesha malumbano kwa muda mrefu. Inadaiwa kuwa majina hayo yote na ya vigogo wengine yamekatwa na jana baadhi yao walikuwa wanadai kuwa CCM kinataka kuzalisha upinzani ambao utakisababishia kushindwa katika safari yake kisiasa hasa katika mfumo huu wa vyama vingi. Licha ya makaripio hayo, Rais Kikwete alibainisha kuwa CCM kinasemwa na watu kuwa kinakithiri rushwa katika chaguzi zake hivyo akawataka wagombea kubadilika kabla ya kukamatwa na Takukuru. “Zipo taarifa ingawa hatujazithibitisha kwamba wapo baadhi ya wagombea wanamwaga fedha sijawahi kuona… Takukuru wapo wanaendelea na kazi. Chama chetu kinasemwa tujipe fursa ya kubadilika, tusisubiri kukamatwa na kuanza kuilaumu PCCB.” 

Kuhusu uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali, Rais Kikwete alisema katika uchaguzi huo, wamejitokeza watu wengi tena vijana wasomi na kwamba Kamati ya Usalama na Maadili na Kamati Kuu, zimewapandisha na kuwakata waliotumikia chama muda mrefu. “Kama hukuteuliwa kuna mawili, ama nafasi zimejaa au hufai una upungufu kidogo na huo ni utaratibu wa chama siyo kuoneana,” alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa. 

Alisema katika uteuzi huo vijana watapewa nafasi zaidi kutokana na ukweli kuwa, chama bila ya vijana hakiwezi kuwa imara kwa sababu ndiyo nguvu ya ushindi. “Hao watakaoachwa watambue kuwa tunafanya hivyo kwa ajili ya kutengeneza timu ya ushindi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa Bara na Visiwani, hivyo kuachwa jina lako isiwe nongwa,” alisema na kuongeza: “Lazima tukipe chama chetu watu wa kushinda… Lazima tutambue sasa tunaunda timu ya ushindi wa chama siyo ushindi wa mtu.” Hata hivyo, Rais Kikwete alitoa angalizo kuwa anajua kikao cha Halmashauri Kuu kingekuwa na mjadala mzito, lakini lazima wakipe chama watu wa kushinda. Majina manne Kamati Kuu ya CCM, inadaiwa kupendekeza majina ya wagombea wanne kwenye jumuiya zake, tofauti na kanuni ya chama hicho ya nafasi moja kuwaniwa na watu watatu. Kikao chake kilichomalizika juzi usiku, kinadaiwa kubadili kanuni ya kupendekeza wagombea watatu kwa nafasi moja na kwamba, hivi sasa mapendekezo hasa kwenye jumuiya ni wagombea wanne. 

 Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa, hatua hiyo inalenga kutoa ushindani kwa wagombea. Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipotakiwa kuzungumzia suala hilo hakukanusha wala kukubali zaidi ya kusema kwamba hata kama utaratibu huo umetumika siyo mara ya kwanza kwa chama hicho. Alisema kama Jumuiya ya Vijana wanaojitokeza lengo lao linakuwa kupata uzoefu na kwamba, idadi ya majina inategemeana na busara za kikao kinavyoona ili kutoa nafasi kwa wagombea kujipima. 
 Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz
BALOZI WA MAREKANI AZINDUA MRADI WA REJEA KWENYE TIBA MJINI IRINGA
Balozi wa Marekani nchini Alfonso E. Lenhardt akiongea na wananchi Iringa mjini siku ya uzinduzi

Maambukizi ya Ukimwi Mkoni Iringa yanakadiriwa kuwa 15.6 % na ni ya juu kabisa nchini ambayo ni mara tatu ya wastani wa Kitaifa. Mradi wa TUNAJALI afya yako umedhamilia kupambana na maambukizi hayo pamoja na kutokomeza kabisa kufikia lengo la kuandikisha na kisha kuwabakiza kwenye huduma na tiba za VVU/UKIMWI zaidi ya watu 20000 wanaoishi na virusi hivyo ili waweze kuishi maisha yenye afya na tija zaidi.

Hayo yamezungumzwa na Balozi wa Marekani Alfonso Lenhardt katika uzinduzi wa mkakati wa “rejea kwenye tiba “ uliofanyika leo katika kituo cha Afya Ipogolo Manispaa ya Iringa. Alisema hivi sasa asilimia 25% ya watu waliokuwa wakitumia ARV wameacha tiba hiyo ambayo ni muhimu na siyo tu kuwaanzishia watu dawa lakini ni muhimu pia kuhakikisha kuwa wagonjwa hao wanabaki katika tiba. “Kiwango hiki cha walioacha dawa kinatutia wasiwasi kuhusu afya na ustawi wa watumiaji na pia kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi katika jamii kwa ujumla,” alisema Lenhardt. 

Kwa mujibu wa mwongozo wa huduma na tiba za VVU na UKIMWI uliofanyiwa marekebisho na kutolewa na Serikali ya Tanzania mapema mwaka huu ambapo kwa sasa mtu anastahili kuanza kutumia ARV wakati CD4 zake zikiwa 350 badala ya 200.

Alisema uzinduzi wa Mkakati huo ni madhubuti kwa kueneza ujumbe wa “pima , endapo umeambukizwa na unastahili kuanza tiba ni vyema ukaanza mapema na endapo umeacha tiba kwa sababu yoyote ile, ni lazima ukarejea kwenda kupata huduma”. Aidha Balozi huyo amesema katika kipindi cha miaka tisa toka 2003 watu wa Marekani kupitia PEPFAR wamewekeza dola za Kimarekani Bilioni 2 kwa ajili ya kupambana na VVU na UKIMWI nchini Tanzania ambao ni uwekezaji katika maisha. Kwa mujibu wa taarifa ya mapambano dhidi ya Ukimwi Mkoani Iringa kwa kipindi cha mwaka 2011/2012 ambapo Iringa imeathirika kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na Mikoa mingine Tanzania ambapo utafiti unaonyesha maambukizi ya VVU na janga la UKIMWI kitaifa uliofanyika mwaka 2007/2008 maambukizo yameongezeka kutoka asilimia 13.4% mwaka 2003/2004 na kufikia asilimia 15.7.

Aidha hatua ya mkakati huo imewezesha Watanzania zaidi ya 300,000 kutumia dawa zinazopunguza makali ya VVU ambapo hivi sasa zaidi ya Watanzania 525,000 hupokea matunzo na huduma mbalimbali zikiwemo huduma za majumbani.
MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA
Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema akihutubia

Mhe. Lema akiwa na Mhe. Joshua Nassari

Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe.Joshua Nassari akihutubia

Kada aliyejitoa CCM Arusha Ally Bananga

REDDS MISS TANZANIA 2012 KUFANYIKA NOV 03 UBUNGO PLAZA



Salha Israel (kulia) akifurahia zawadi yake ya gari aina ya Jeep wakati akikabidhiwa mwaka jana chini ya wadhamini wa waliopita kampuni ya huduma za simu ya Vodacom. Shindano hilo sasa linadhaminiwa na bia ya Redds.

Salha Israel (wa pili kushoto) akifurahia zawadi yake ya gari aina ya Jeep wakati akikabidhiwa mwaka jana chini ya wadhamini wa waliopita kampuni ya huduma za simu ya Vodacom. Shindano hilo sasa linadhaminiwa na bia ya Redds.

Salha Israel akiwa katika bango la Redds Miss Tanzania 2012 wakati wa uzinduzi wa shindano la mwaka huu


SHINDANO la Redds Miss Tanzania 2012 litafanyika Novemba 3 kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, waandaaji kamati wa Miss Tanzania wametangaza leo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam, mratibu wa shindano hilo, Hashim Lundenga, amesema warembo wataingia kambini Oktoba 2 katika hoteli ya Giraffe, ambako watakaa hadi siku ya shindano.
  
Mshindi wa shindano hilo atamrithi, Salha Israel kutoka Ilala anayeshikilia taji la taifa. Kwa kushinda shindano hilo mwaka jana, Salha alizawadiwa gari kali aina ya Jeep.

Hata hivyo, mapema mwaka huu kamati hiyo iliendesha shindano dogo na kumpata Lissa Jensen ambaye aliwakilisha nchi katika fainali za Dunia kutokana na mabadiliko ya kalenda yaliyofanywa na Kamati ya Miss World.

Miss Tanzania atakayepatikana Novemba 3 atakuwa na muda mrefu wa kujiandaa na atashiriki katika shindano la Miss World la mwakani na utaratibu huo utakuwa wa kudumu.

Hadi sasa, Miss Tanzania aliyepata mafanikio katika shindano hilo la dunia ni Nancy Sumary ambaye alitwaa taji la Miss World Africa 2005.

Tuesday, September 25, 2012

KATIBU MKUU WA APRM AONGEA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR
Katibu Mtendaji wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora(APRM) Tawi la Tanzania Rehema Twalib (kulia) akiongea na waandishi wa habari jana(leo)  mjini Dar es salaam kuhusu mafunzo ya Maofisa Mipango wa serikali yanayolenga kuwaelimisha jinsi ya kusimamia na kuoanisha utekelezaji wa maoni ya watanzania kuhusu utawala bora. Mafunzo hayo yanaanza kesho tarehe 25 septemba 2012 mjini Dar es salam.Katikati ni Mratibu wa APRM kutoka Makao Makuu Dr. Rachel Mukamunana na kushoto Afisa anayeshughulikia masuala ya APRM na NEPAD kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa UNDP Zemenay Lakew .

Picha na Veronica Kazimoto- MAELEZO- Dar es salaam
CHADEMA YAKATAA KUKUTANA NA KAMATI YA NCHIMBI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KATIKA
 kusimamia uongozi unaozingatia misingi muhimu ya haki za binadamu, sheria na utawala bora, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesisitiza msimamo wake wa kutotoa ushirikiano kwa kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi kuchunguza kifo cha Mwandishi wa Habari wa Channel ten, Daudi Mwangosi, kilichotokea Septemba 2, 2012, Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa. Msisitizo huo umekuja baada ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo kukiandikia barua (isiyokuwa na Kumbukumbu Namba) CHADEMA, akiomba kamati yake ikutane na viongozi wa chama Septemba 25, ili kutafakari tukio hilo na matukio ya aina hiyo yaliyowahi kutokea hapa nchini. 

Itakumbukwa kuwa Marehemu Mwangosi aliuwawa na Jeshi la Polisi akiwajibika kwa jamii katika shughuli za uandishi wa habari, wakati askari wa jeshi hilo walipovamia ofisi za CHADEMA Kata ya Nyololo na kuanzisha vurugu wakati wanachama walipokuwa wakiendelea na shughuli halali za ndani za chama. Katika barua kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, CHADEMA kimesema wazi kuwa hakiko tayari kukaa na kutafakari juu ya kifo cha Mwangosi kama ilivyopendekezwa na kamati hiyo, kwani imeundwa kinyume cha sheria, huku pia ikiwa imeundwa na mtu ambaye kanuni za msingi za utawala bora, zinamtaka awe amejiuzulu au kufukuzwa kazi, kupisha uchunguzi huru juu ya mauaji hayo yaliyofanywa na jeshi la polisi, linalowajibika kwake kama Waziri wa Mambo ya Ndani. Kamati hiyo pia inawahusisha polisi ambao katika tukio hilo ni watuhumiwa namba moja.

 Mbali ya kusisitiza kuwa haiwezi kutoa ushirikiano kwa kamati ambayo haipo kwa mujibu wa sheria, CHADEMA kimeshangazwa na kusudio hilo la Kamati ya Nchimbi kutoa mwaliko wa kutaka kukutana na viongozi wa CHADEMA, huku ikitambua wazi msimamo wa chama hiki juu ya uwepo wa kamati hiyo mara tu ilipoundwa.  Kutoa ushirikiano kwa kamati ambayo haina mamlaka ya kisheria ya kuhakikisha ukweli mtupu unajulikana na haki ionekane ikitendeka kutokana na kifo hicho na vingine vingi ambavyo vimefanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia, kwa masuala mbalimbali yakiwemo ya kisiasa, ni kuhalalisha uvunjivu wa haki za binadamu, Katiba na sheria za nchi. CHADEMA haiko tayari kuona hali hiyo ikifanyika. 
  Katika kuonesha msisitizo wa kutokubali mwaliko wa Kamati ya Nchimbi inayotaka kutafakari matukio ya vifo ambapo Jeshi la Polisi limewanyang’anya watu wasio na hatia haki ya kuishi, katika barua yake ya majibu, CHADEMA pia kimeambatanisha nakala ya barua ya tarehe 10/09/2012 iliyowasilishwa kwa Rais, ili kamati hiyo iweze kuelewa msimamo mpana wa chama kuhusu mauaji ya kisiasa yanayofanyika nchini. Kwa taarifa hii, CHADEMA kinaendelea kusisitiza maazimio ya Kamati Kuu ya Chama, ambayo pamoja na mambo mengine, iliazimia kuwa kutokana na mfululizo wa matukio ya mauaji ya kisiasa yanayofanywa na Jeshi la Polisi katika shughuli halali za chama, Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile wawajibike kwa kujiuzulu au Rais awawajibishe kwa kuwafukuza kazi ili wapishe uchunguzi huru na wa haki. 
 Pia Kamanda wa Polisi Iringa, Michael Kamuhanda, Kamanda wa FFU Mkoa wa Morogoro, na askari wote wanaoonekana kwenye picha wakiwa wamemzunguka Mwangosi muda mfupi kabla hajalipuliwa na kuuwawa, wakamatwe haraka na kushtakiwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Mwangosi. 

Kinyume na hapo ni kuchezea akili za wapenda haki na uwajibikaji, ikiwa moja ya misingi ya amani Tanzania na dunia nzima kwa ujumla.

 CHADEMA inapenda kusisitiza kuwa itatoa ushirikiano kwa chombo kitachoundwa kwa mujibu wa Sheria huku ikitilia msisitizo wito kwa Rais kuunda Tume ya Kimahakama/Kijaji kuchunguza vifo vyote vyenye utata na vinavyohusishwa na masuala ya kisiasa kama tulivyopendekeza kwake hapo kabla.  Imetolewa leo Septemba 24, 2012 Dar es Salaam na;
DK. MIGIRO AFUNGUA MKUTANO WA SERIKALI ZA MITAA JIJINI ARUSHA
Dk.Asha Rose Migiro akifungua mkutano wa mawaziri wa serikali za mitaa wa Afrika Mashariki kwenye hoteli ya Impala mjini Arusha


























































Naibu Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake,Dr Asha-Rose Migiro(wa nne kulia)akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja baada ya kufungua mkutano wa mawaziri wa serikali za mitaa wa Afrika Mashariki mjini Arusha.

Monday, September 24, 2012

KINANA ANG'ATUKA CCM


 Kada maarufu wa CCM Abdulrahaman Kinana


NI BADA YA KUWA MJUMBE NEC, KAMATI KUU KWA MIAKA 25, AZUNGUMZIA UCHAGUZI 2015, HATIMA YAKE BAADA YA SIASA 

 KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana ametangaza kung’atuka rasmi katika siasa baada ya kukitumia chama chake kwa miaka 25 akiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Kamati Kuu (CC) na Kamati ya Maadili. Kinana ambaye amekuwa Meneja wa Kampeni za mgombea urais wa CCM tangu mwaka 1995 ulipoanza uchaguzi wa vyama vingi, alisema kwamba baada ya kutumikia chama katika nyadhifa za juu kwa robo karne sasa, ameamua kupumzika ili kuwaachia vijana waendelee kukijenga chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika.

 “Nimekuwa Mjumbe wa NEC kwa miaka 25, bila shaka muda huu unatosha, kwani wanaCCM wamenipa heshima ya kuwa katika vikao vya juu vya chama kwa robo karne. Sasa ni wakati wa kung’atuka, nimetoa mchango kwa kadri nilivyoweza katika vikao mbalimbali na katika shughuli nyingi,” alisema. Alisema anaamini kuachana kwake na siasa hakutakuwa na madhara kwa chama chake, kwani CCM ina hazina kubwa ya viongozi ambao wana sifa na wanaweza kuongoza chama hicho kuelekea Uchaguzi wa 2015.

 “Uongozi ni kupokezana vijiti. Wako wanaCCM wazuri, walio na uwezo mkubwa na sifa za kutosha kuongoza. Nawashukuru wanaCCM na viongozi kwa heshima waliyonipa wakati wote huu,” alisema Kinana ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni wa Rais Benjamin Mkapa kwa vipindi viwili na Rais Jakaya Kikwete kwa vipindi viwili vya uchaguzi. Kinana alisema anajivunia kufanya kazi na marais wote wa Tanzania kuanzia Mwalimu Julius Nyerere hadi Rais Kikwete kwa uadilifu mkubwa na kuheshimiana.

 ”Ushauri wangu katika vikao umekuwa ukiheshimika sana. Nimekuwa nikiheshimiwa na uongozi wote wa CCM na hata wapinzani nao tunaheshimiana. Nimesimamia kampeni za kistaarabu na ambazo zimeleta ushindi mkubwa kwa CCM tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi,” alisema. Kinana ambaye pia alikuwa Spika wa Kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), ameshauri vijana ndani ya CCM watangulize masilahi ya taifa mbele na wasikilize wananchi. Ni muhimu washikamane, wabuni mikakati ya kusaidia kukuza uchumi kwa haraka zaidi na kuendeleza umoja na undugu wetu,” alisema. 

Ushauri wa viongozi wapya CCM Kinana alishauri viongozi wapya ambao wanatarajiwa kuchaguliwa ndani ya chama chake, iwapo wataona upungufu wake wausahihishe. “Ni matumaini yangu kuwa watakaopata uongozi wataona upungufu na watasahihisha makosa yangu,” alisema. Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2015, Kinana aliwaasa viongozi wasiwaze nani anafaa kuwa mgombea urais bali washughulikie kero za wananchi. 

 “Bado tuna kazi kubwa ya kutekeleza Ilani. Tusiwasumbue Watanzania kuwa ni nani anafaa kuwa Rais bali tushughulikie matatizo yao. Kwa sasa ajenda ya CCM ni kutekeleza ahadi zetu katika sekta zote siyo kutafuta nani atakuwa Rais 2015," alisema na kuongeza: 

"Hata wapinzani wawaeleze Watanzania yale ambao wamedhamiria kutekeleza. Kueleza upungufu wa CCM ni mtaji mdogo kwa wapinzani, ajenda kubwa ni watafanya nini? Hapa bado wana kazi kubwa. Wanapoona upungufu wasisite kutusema,” Kinana ambaye ana shahada ya uzamili katika utawala na masuala ya sera kutoka Chuo Kikuu cha Harvad nchini Marekani, alisema anatarajia kufundisha na kusoma Shahada ya Uzamivu (PhD) katika moja ya vyuo vikuu vya hapa nchini.

 “Baada ya kustaafu kuna mambo mawili ambayo natarajia kufanya. La kwanza ni kuona kama naweza kufundisha. Pili kusoma katika mojawapo ya vyuo vikuu vyetu,” alisema. Mbali na nyadhifa zilizotajwa huko juu, Kinana ametumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa muda mrefu na kupanda cheo hadi kufikia Kanali. Amewahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mbunge wa Arusha Mjini. 

Nape alisema Kinana ni miongoni mwa wanasiasa waadilifu wa CCM ambao wamekitumikia chama kwa muda mrefu na kwa uaminifu wa hali ya juu. Ni kweli hajagombea, lakini kutokugombea kwake hakujafungwa milango kwa CCM kumtumia au kutumia uzoefu wake pale watakapomhitaji. Alisema "Kwa mfano Mwenyekiti wa CCM ana nafasi alizopewa kikatiba kuteua wajumbe wa NEC, huwezi kujua anaweza akamwona anafaa na akamteua," 

Chanzo: www.mwananchi.co.tz 

Sunday, September 23, 2012

WIKI YA NENDA KWA USALAMA YAMALIZIKA

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya nenda kwa usalama Mkoa wa Iringa Salim Abri Asas mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Samora Mkoani Iringa kufunga maadhimisho hayo 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa akisalimiana na RPC wa Mkoa wa Mbeya Bw. Diwani Athuman mara baada ya kuwasili katika uwanja huo




























Wabunge wa Viti Maalum wakiwa katika Maadhimisho hayo.





























MKUTANO JUU YA SERA YA KUDHIBITI POMBE KUFANYIKA TANZANIA
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi




































 MKUTANO wa Kimataifa kujadili umuhimu wa nchi za Afrika Mashariki kuwa na sera ya kudhibiti ulevi unaanza Arusha kesho. Mkutano huo wa siku mbili utakaofanyika katika hoteli ya Naura Springs utahudhuriwa na watu 80 ambao kwa namna moja au nyingine kazi zao zinaguswa na madhara ya ulevi. Mkutano huo wenye kauli mbiu “Ulevi ni matatizo chukua hatua sasa” utafunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi.

 Balozi wa Sweden nchini Dk. Lennrth Hjelmaker atatoa mada kuu kuhusu madhara ya ulevi na jinsi ya kuwa na umuhimu wa kuwa na sera ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe. Ulevi una madhara makubwa kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuchochea migogoro majumbani na kusababisha ajali zinazouwa watu wengi na kuacha wengine vilema. Washiriki wa mkutano huo wanatoka nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi, Sweden, Norway na Tanzania. 

Mada zitakazowasilishwa katika mkutano huo ni pamoja na zile zitakazojadili hatua zilizofikiwa na nchi za Afrika Mashariki katika kuweka sera ya kudhibiti vilevi. Mwakilishi wa Malawi ambaye nchi yake imechukua hatua kutunga sera ya kudhibiti ulevi atawasilisha mada kuzungumzia fursa na changamoto zake. Siku ya pili mkutano huo utafanya warsha nne ambazo zitazungumzia mada mbalimbali zote zikilenga kuelimisha na kuhamasisha washiriki kuona umuhimu wa nchi za Afrika Mashariki kuwa na sera ya kudhibiti ulevi. 

Mkutano huo umeandaliwa na Shirika la Kimataifa lisilokuwa la Kiserikali IOGT ambalo linahamasisha maendeleo kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kijamii Afrika ya Mashariki. Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani hapa nchini Dk. Neema Kileo na mwakilishi IOGT katika ngazi ya kimataifa Kristina Sperkova watatoa ujumbe maalum kwenye mkutano huo. Mkutano huo utafungwa rasmi na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dk. Richard Sezibera.

 Chanzo: http://www.thehabari.com

Friday, September 21, 2012

HIVI NDIVYO CHADEMA WLIVYOJITOKEZA KESI YA GODBLESS LEMA MJINI ARUSHA JANA





Thursday, September 20, 2012

JAJI MKUU AAPISHA MAHAKIMU
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman akiwaapisha mahakimu 372 wakiohitimu kwenye chuo cha mahakama huko Lushoto.



















KERO YA USAFIRI JIJINI DAR ES SALAAM
Abiria wakiwa wanasukumana wakitaka kuingia kwenye daladala asubuhi ya leo huko Tabata , Adha ya usafiri jijini imeshamili.


























HAYA NDIO MABASI MAPYA YA KISASA YA TIMU YA SIMBA NA YANGA WATAKAYOPEWA NA WADHAMINI WAO

 KAMPUNI ya Bia Tanzania kupitia Bia ya Kilimanjaro Premium Lager hatimaye inatarajia kukabidhi mabasi mapya ya kisasa kwa timu za Simba na Yanga siku ya Ijumaa asubuhi.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na makabidhiano hayo yatafanyika katika viwanja vya ofisi za TBL Ilala.

“Zaidi ya wageni 100 wamealikwa kwenye hafla hii itakayofanyika Ijumaa hapa TBL na kati ya hawa wageni kutakuwa na baadhi ya mashabiki wa timu hizi mbili kwa hivyo tunatarajia makabidhiano ya aina yake,” alisema Kavishe.

Kwa mujibu wa ratiba, baada ya makabidhiano, kila timu itaondoka na basi lake na wachezaji na mashabiki na kupita katika matawi yao kwa msafara maalumu utakaoambatana na burudani mbalimbali huku mashabiki wa timu hizi wakitarajiwa kuyapokea mabasi hayo na kuwashangilia wachezaji wakipita katika matawi.

Msafara wa timu ya Simba ukiondoka TBL Ilala utaelekea katika Tawi la Vuvuzela lililopo Makao Makuu ya klabu hiyo Kariakoo Mtaa wa Msimbazi kisha utaelekea katika Tawi la Magomeni Mpira Pesa, Ubungo katika kituo cha mabasi na hatimaye Tawi la Wailes Temeke.

Msafara wa Yanga nao ukiondoka TBL Ilala utaelekea katika Tawi la Ubungo katika kituo cha mabasi na kuelekea katika Tawi la Manzese, Lango la Jiji Magomeni, Buguruni, Mwembe Yanga, Mtoni kwa Aziz Ali, Mkombozi na hatimaye kumalizia katika makao makuu ya Jangwani, Kariakoo.

"Tunawaomba mashabiki wa timu hizi mbili wajitokeze kwa wingi katika matawi yao ili wajionee mabasi haya mapya ambayo ni ya kisasa na pia wapate fursa ya kukutana na wachezaji wa timu zao," alisema Kavishe.

Kilimanjaro Premium Lager imedhamini klabu hizi hivi tangu mwaka 2008.


Source/http://straikamkali.blogspot.com/

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YATOA MAAGIZO
Naibu waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele akitoa maagizo alipotembelea ofisi za TMAA, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TMAA, Bw. Paul Masanja.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Stephen Masele ameiagiza Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) kuimarisha ukaguzi maeneo ya migodini hususan maeneo ya migodi mikubwa.

Mhe.Maselle alitoa agizo hilo alipotembelea ofisi za Wakala zilizopo maeneo ya Kurasini jijini Dar es Salaam.
Alibainisha kuwa TMAA haina wakaguzi ambao wanakuwa ndani ya mashimo ya migodi hiyo hivyo kuna umuhimu wa kuwa na mkaguzi mwingine ambaye atakuwa maalumu kwa ajili ya kufanya ukaguzi ndani ya mashimo.

“Ugakuzi makini utahusika pia na kuhakiki gharama za uwekezaji na uendeshaji wa migodi mikubwa ya ili kudhibiti mapato ya Serikali”, alisema Masele na kuongeza kuwa madini yanayosafirishwa kwa mashine kutoka katika mashimo ni kiasi kidogo tofauti na yale ambayo yanatolewa kwa kuokotwa kwa mkono kutoka huko katika mashimo.

Aidha, Naibu Waziri huyo aliipongeza TMAA kwa kufanikisha kukamatwa kwa mameneja watatu wa Kampuni ya Aureus Ltd ambao wanatuhumiwa kukwepa kodi na kutorosha dhahabu nje ya nchi. “TMAA ni jicho la Wizara, mmefanya ukaguzi na mmebaini haya, endeleeni hivyo hivyo, taarifa zote mtakazoleta tutazifanyia kazi”, alisisitiza.
Alisema ukaguzi uliofanywa na TMAA unaonesha uzalishaji wa kampuni hiyo ni mkubwa kuliko uliokuwepo kabla ya kuanza kwa ukaguzi. “Tukigundua vitendo vya utoroshaji ama ukwepaji wa kulipa mapato kwa namna yoyote, tutachukua hatua kali ili iwe ni fundisho kwa wengine wenye tabia za namna hii” alionya.

Naye Mtendaji Mkuu wa TMAA, Paul Masanja alisema TMAA itaendelea kufanya kazi kwa kasi zaidi ili kuendelea kuwabaini wale wote wasiyowaaminifu na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake.
 
“Tunakuahidi Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba sisi hatutorudi nyuma, tutaendelea kutoa ushirikiano wa karibu zaidi na tutafanya kazi zetu kwa ufanisi ili kufikia malengo” aliongeza. 

JK AMTEUA RISHED BADE KUWA NAIBU KAMISHNA MKUU WA TRA
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished Bade (pichani) kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Taarifa hiyo ilitolewa Jumatano Septemba 19,2012 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais - Ikulu , imesema kuwa uteuzi huo umeanza jumatatu wiki hii Septemba 17,2012.
Kabla ya uteuzi wake Bwana Bade alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Mortage Finance CO.LTD

DKT . MWELE MALECELA ATUNUKIWA TUZO YA MAPAMBANO DHIDI YA MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE
Dkt. Mwele Malecela (Pichani) ametunukiwa tuzo ya NTD Champion Awards huko Wishington Marekani kwa kazi yake ya mapambano dhidi ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele. Dkt Malecela alipewa tuzo hiyo katika hafla maalum iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Maseneta na wawakilishi wa Congress Akimtunikia tuzo hiyo Naibu Mkuu wa wa USAID anayeshughulikia Afya Dr. Areil Pabloz - Mendez alisifia mchango mkubwa wa Dkt. Malecela Kitaifa na Kimataifa katika kupambana na magonjwa hayo.

Wednesday, September 19, 2012

MABINGWA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI YANGA WALALA 3-0























Dar es Salaam Young Africans wameendeleza mwanzo mbaya wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 toka kwa wakata miwa Mtibwa Sugar. Wakati huo Mnyama ameendelea kuunguruma uwanja wa Taifa baada kuichapa JKT Ruvu 2-0 Kwa mabao ya Amri Kiemba na Haruna Moshi Boban, pamoja na kucheza pungufu baada ya Emmanuel Okwi kupewa kadi nyekundu kipindi cha kwanza.
TAMKO LA SERIKALI JUU YA GHASIA ZA UCHAGUZI MDOGO BUBUBU- ZANZIBAR
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema hakuna mtu aliyefariki kutokana na vurugu siku ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu uliofanyika Jumapili iliyopita kama ililivyodaiwa na gazeti moja linalotolewa kila wiki hapa nchini.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar na kutiwa saini na waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed imeeleza hadi sasa hakuna taarifa yoyote ya kifo kilicho sababbishwa na vurugu hilo iliyoripotiwa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa jeshi la Polisi lilipokea taarifa ya kujeruhiwa watu kutokana na vurugu za baadhi ya vikundi vya wananchi vilivyojipanga kuwazuia wananchi wengine kwa makusudi kushiriki katika zoezi la kupiga kura.
Kuhusu tuhuma zilizo tolewa dhidi ya Makamo wa Pili wa Rais katika zoezi la upigaji kura taarifa hiyo ilieleza kuwa maelezo hayo siyo ya kweli na kwamba zinalenga kumchafulia jina Kiongozi huyo wa ngazi za juu

Kufuatia tuhuma hizo Serikali imemtaka Mhariri wa Gazeti la FAHAMU kuthibitisha kwa maandishi tuhuma walizoandika dhidi ya Mheshimiwa Makamo wa Pili wa Rais au kumuomba radhi kwa maandishi kupitia Gazeti lake la FAHAMU katika kipindi kisichozidi siku saba(7) kuanzia tarehe ya taarifa hii. Vyenginevyo Serikali itachukuwa hatua zinazofaa dhidi ya wahisika wote.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kusikitishwa kwake na taarifa zilizotolewa na kiongozi mmoja wa Ngazi za juu wa CUF kupitia gazeti hilo kwa kumtaja Makamo wa Pili wa Rais kuwa kiongozi wa juu wa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar aliyejitosa kuharibu matokeo ya kura kwa kuingia katika baadhi ya vituo kama kiongozi wa Wawananchi.

Tuhuma hizo si za kweli na zisingepaswa kutolewa na Kiongozi wa juu wa chama cha siasa kwani kiongozi huyo anaelewa fika kwamba tuhuma hizo zinachafua jina la kiongozi huyo na kuhatarisha Umoja wa Taifa Letu.

          IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 19/09/2012.