WAZIRI WA FEDHA SAADA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KARIAKOO NA MTAA WA NAMANGA
Waziri wa
Fedha Saada Mkuya Salum (wa pili kulia) akiongoza na viongozi wa mkoa
wa kodi wa Ilala kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na
maafisa wa Serikali alipofanya ziara ya kushtukiza leo jijini Dar es
salaam katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara
wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD
ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia
Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini.
Wa kwanza kulia ni Kaimu Msaidizi wa Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala
kutoka TRA Hamidu Athmani, wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa mkoa wa
kodi wa Ilala Elias Balongo na kushoto mwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda (wa kwanza kushoto)
akiteta jambo na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa pili kushoto)
katika ziara ya kushtukiza katika soko la Kariakoo kujionea namna
wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za
kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa
zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma
za jamii nchini. Aliyevaa tai kulia ni wa kwanza kulia ni Kaimu
Msaidizi wa Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA Hamidu Athmani.
Wananchi
wakifuatilia ziara ya kushtukiza ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum
aliyofanya leo jijini Dar es salaam katika soko la Kariakoo kujionea
namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine
za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza
bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa
huduma za jamii nchini.
No comments:
Post a Comment