TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, January 21, 2015

TEMBO, SIMBA WASIOFUGIKA WANUSURIKA AFCON 

Doumbia-Inaction-150120SS720
MIAMBA ya soka kutoka Magharibi mwa Afrika, Ivory Coast imeanza kwa sare ya 1-1 dhidi ya Guinea katika mechi ya kundi D , michuano ya mataifa ya Afrika inayoendelea huko Guinea ya Ikweta.
Guinea walikuwa wa kwanza kufunga goli katika dakika 36' kipindi cha kwanza kupitia kwa nyota wake Mohamed Yattara, hata hivyo Ivory Coasta walisawazisha dakika ya 72' kupitia kwa Seydou Doumbia.
Nayo mechi ya pili ya kundi kund hilo baina ya Mali na Cameroon imemalizika kwa sare ya 1-1.(P.T)
Mali waliandika bao la kuongoza dakika ya 71' kupitia kwa Yambou Yatabare, lakini Simba wasiofugika, Cameroon wakasawazisha kupitia kwa Ambroise Oyongo Bitolo.
Kufuatia kumalizika kwa mechi za kwanza za kundi D, michuano hiyo leo inaendelea kwa mzunguko wa pili wa makundi.
Timu za kundi A zinaanza kutupa karata yao ya pili ambapo mechi ya kwanza itawakutanisha wenyeji Guinea ya Ikweta dhidi ya Burkinafaso ambao walipoteza mechi ya kwanza kwa mabao 2-0 dhidi ya Gabon.
Mechi ya pili inayoanza majira ya saa 4:00 usiku leo, itawakutanisha Congo na Gabon.
Chanzo:Shaffihdauda

No comments:

Post a Comment