CAMERON :NI SAWA NA MAGAZETI KUKERA
Waziri
Mkuu wa Uingereza, David Cameron, amepinga matamshi ya Papa ya juma
lilopita aliposema kuwa siyo sawa kufanya mzaha juu ya imani ya watu
wengine.
Akijibu
kuhusu mashambulio yaliyofanywa na wapiganaji Waislamu dhidi ya gazeti
la Ufaransa la Charlie Hebdo, Papa alisema iwapo mtu atamtusi mama ake,
ataraji ngumi.
Bwana Cameron hata hivyo alisema katika nchi huru kuna haki ya kukera kuhusu dini ya mtu mwengine.
Aliliambia
shirika la habari la CBS la Marekani, kwamba vyombo vya habari vinafaa
kuweza kuchapisha vitu ambavyo vinawakera baadhi ya watu - ikiwa siyo
kinyume na sheria.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment