Kuhusu ile ishu ya Wanafunzi kupigwa mabomu ya machozi Kenya, iko hapa kauli ya Rais Kenyatta
Waziri wa usalama nchini Kenya, Joseph Nkaissery
amewaomba radhi wanafunzi wa shule ya msingi ya Lang’ata baada ya
kupigwa mabomu ya machozi jana walipoandamana kupinga kunyang’anywa
kipande cha ardhi ambacho kilikuwa uwanja wao wa kuchezea.
“Jana hata hawataki tusherehekee, tukicheza wanatupiga na rungu wanatuletea madogi”– Mwanafunzi.
Rais Uhuru Kenyatta amelaani tukio hilo na kumtaka Waziri wa Ardhi, Charity Ngilu na Mwenyekiti wa Tume ya Ardhi, Mohammed Swazuri kuwajibika
na kueleza kwanini walizembea, huku Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo pia
kalaumiwa kwa kusindwa kuzuia watoto hao kujihusisha na vurugu.
Bado haijafahamika ni nani aliyehusika na ujenzi huo.
No comments:
Post a Comment