TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, January 14, 2015

Gavana kaamua kupiga marufuku matumizi ya lift ili kupambana na tatizo la uzito mkubwa!

Obesity
Majengo mengi yaliyo katika ghorofa kuanzia nne na kuendelea yamekuwa yakiwekwa lift za umeme ili kusaidia watu kupanda na kushuka kwa urahisi na uharaka, nimekutana na hii story ya Gavana mmoja kuzuia watu kutumia lift ili watu wapambane na tatizo la uzito mkubwa.
elevator-pitch
Obesity imekuwa moja ya tatizo linalowakabili sana watu wa nchi za Ulaya, mwaka jana Uingereza na Hungary zilitajwa kama moja ya nchi zenye tatizo hili kwa kiasi kikubwa.
Hii ilikuwa takwimu ya tatizo la Obesity mwaka 2014 kwa wenye umri wa miaka 15 na zaidi nchi za Ulaya.
Dursun Ali Sahin, Gavana wa Jimbo la Edirne, Uturuki amepiga marufuku hiyo ili watu watumie ngazi kupanda kuanzia ghorofa ya kwanza mpaka ya tatu, ila watakaoruhusiwa ni wale tu ambao wana matatizo ya kiafya.
Majengo ambayo hayajaguswa katika agizo hilo ni Hospitali na kwenye nyumba za wauguzi peke yake.
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Ukitumia ngazi badala ya lift inakuongezea siku za kuishi… Hii ni hatua ya kupromote afya bora… Itasaidia pia kupunguza gharama za matumizi ya umeme…” – Sahin.
Mwaka jana Gavana huyo aliwahi kupiga marufuku matumizi ya sukari kwa wingi katika chai zinazouzwa katika migahawa.
Mitandao ya kijamii haijakosa kuzungumzia hili, watu waliopita huko wamesema eti ujanja utakaotumika utakuwa hivi; mtu akiwa na shida ghorofa ya tatu atajirahisishia safari yake, atapanda lift mpaka ghorofa ya nne halafu atafanya kutembea tu kurudi ghorofa ya tatu kwa kushuka ngazi.

No comments:

Post a Comment