RIPOTI KAMILI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KUJULIKANA LEO

Mwenyekiti
 wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya 
Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza jambo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya 
CCM,Ndugu Adam Kimbisa,wakati akitoka nje mara baada ya kumaliza kikao 
cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa usiku huu,kilichofanyika jana 
katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja,Zanzibar,kikao hicho
 kilianza mnamo majira ya saa sita mchana na kumalizika usiku mnamo saa 
mbili na ushehe hivi huku mambo mbalimbali yakiwa yamejadiliwa ikiwemo 
suala la sakata la Akaunti ya Escrow,Hali ya kisiasa nchini,uchaguzi 
Mkuu na mambo ya Maadili na mengineyo.

Pichani 
ni Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Wanahabari
 usiku wa kuamkia leo baada ya kikao cha kamati kuu cha CCM kuisha nje 
ya ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Unguja kisiwani 
Zanzibar.Nape ameeleza kuwa taarifa rasmi ya yaliyohusu kikao hicho 
atayaweka wazi mapema leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment