Wanamgambo wa Kishia walivamia Ikulu ya rais
Vizuizi
vya kikosi kinachotoa ulinzi wa taasisi za nchi kwenye barabara
inayoelekea kwenye Ikulu ya rais katika mji wa Sanaa, Januari 20 mwaka
2015.
Na RFI
Kwa
mujibu wa afisa wa kijeshi aliyenukuliwa na shirika la habari la
Ufaransa AFP, wanamgambo wa Kishia waliokua wameizingira Ikulu ya rais,
wameendesha mashambulizi na kwa sasa wanadhibiti boma la rais.
Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mkutano wa dharura bila hata
hivyo kutomriuhusu mtu yeyote asiyekua muhusika kushiriki mkutano huo.(P.T)
Kulingana na vyanzo viliyonukuliwa na mashirika ya habari Reuters na AFP, wanamgambo wa Kishia waliitdhibiti Ikulu ya rais.
Inaonekana
kuwa kikosi kilichokua kinatoa ulinzi wa rais kilindoka katika eneo
hilo kabla ya kushambuliwa na wanamgambo hao wa Kishia.
Mapigano
yanaendelea karibu na boma la rais wa Yemen, bila hata hivyo kujua
hatima ya rais, Abd Rabbo Mansour Hadi. Wakati huohuo, makazi ya Waziri
Mkuu bado yanaendelea kuzingirwa na watu wenye silaha wakizuia barabara
kuu inazoelekea kwenye makaazi hayo.
Miezi
minne baada ya kuingia katika mji mkuu wa Yemen, inaonekana kuwa
wanamgambo wa Ansaroullah wameamua kuongeza nguvu dhidi ya utawala
uliopo sasa, huku wakiendelea kudhibiti maeneo muhimu ya mji mkuu wa
Yemen. Kwa kutaka kutetea hoja yao, wanamgambo wa Kishia wanalani
muswada wa Katiba, wakibaini kwamba unawakandamiza raia.
Kulingana
na waangalizi wengi, wanamgambo wa Kishia, katika mashambulizi yao
mapya wanaufaika na msaada kutoka moja kwa moja kwa wafuasi wa rais wa
zamani wa Yemen, Ali Abdullah Saleh, ambaye alitimuliwa madarakani mwaka
2012 baada ya kuongoza Yemen kwa miongo mitatu.
No comments:
Post a Comment