TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, January 20, 2015

Nimekuletea taarifa hii ya matumaini kwa watu wa Mali kuhusu Ugonjwa wa Ebola

ebola_3022684b 
Mwaka 2014 haukuwa mwaka wenye story nzuri kutoka nchi za Afrika Magharibi kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola watu zaidi ya elfu kumi walifariki na wengine zaidi ya elfu tano wakiripotiwa kuugua ugonjwa huo.
Umoja ya Mataifa na Serikali ya Mali wametangaza kuwa nchi hiyo haina tena ugonjwa hatari  wa Ebola baada ya kutoripotiwa taarifa za mgonjwa yeyote wa Ebola kwa muda wa siku kipindi cha siku 42 zilizopita.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na Ebola ulioandikwa katika ukurasa wa Twitter unawashukuru wafanyakazi wa Afya waliojitolea kupambana na Ebola nchini Mali kwa kuhakikisha ugonjwa huo umedhibitiwa.
Mbali na Mali kuonekana kuathiriwa na ugonjwa huo, Guinea, Sierra leone na Liberia ni mataifa ambayo yamepata athari kubwa kutokana na ugonjwa huo.
Waziri wa Afya wa Mali amewasifu wahudumu wa Afya  na washirika wa Kimataifa kwa msaada wao.

No comments:

Post a Comment