Mwaka mmoja umepita tangu afariki mtangazaji Komla Dumor, BBC imeandaa kumbukumbu hii.
Mwaka
mmoja umepita tangu afariki Komla Dumor, mmoja ya watangazaji maarufu
sana wa kituo cha BBC, alikuwa akiendesha kipindi cha Focus on Africa.
Shirika la habari la BBC
limetangaza kuandaa Tuzo kwa heshima ya mtangazaji huyo mwaka mmoja
baada ya kifo chake kilichotokea January 18, 2014 London na kuzikwa
January 22 nyumbani kwao Accra, Ghana.
Dumor alikuwa
mwandishi na mtangazaji mwenye kipaji cha kipekee kutoka Ghana, huku
akisifika Afrika na duniani kote kwa kufanya kazi kwa kujitolea ambapo
alikuwa akitoa taswira tofauti kuhusu Afrika kwa dunia nzima.
Shirika la BBC limejitolea kuendeleza kazi ya Komla
kwa kutangaza tuzo ya uandishi wa habari kwa heshima kama mwandishi
mahiri, Tuzo itakayokuwa ikitolewa kwa waandishi wenye kipaji cha hali
ya juu.
Hizi ni picha za kumbukumbu ya mwaka mmoja iliyofanyika January 18 nyumbani kwao, Accra Ghana.
No comments:
Post a Comment