BALOZI SEIF ASHIRIKI HARAMBEE CHUO CHA CBE

Makamu wa
 Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd akikabidhi mchango wake 
wa shilingi milioni 3 kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Chuo cha 
Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Mathew Luhanga (katikati) kusaidia 
uboreshaji wa miundombinu ya chuo hicho jana usiku wakati wa harambee 
maalum ya ukusanyaji wa fedha iliyofanyika Hotel ya Serena jijini Dar es
 salamm.Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho

Makamu wa
 Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd na viongozi wa Chuo cha 
CBE wakitoa mkono wa shukrani kwa wadau mbalimbali waliotoa michango yao
 wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya chuo cha CBE jana usiku 
jijini Dar es salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya 
chuo hicho .

Makamu wa
 Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd akisoma majumuisho ya 
michango na ahadi zilizotolewa na wadau mbalimbali waliohudhuria 
harambee ya kuchangia maendeleo ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jana
 usiku jijini Dar es salaam. Kiasi cha shilingi milioni mia tano 
arobaini, laki nane na elfu ishrini na tisa (540,829,000/=) zikiwa ni 
ahadi na fedha taslimu zilikusanywa.
No comments:
Post a Comment