AFCON:KUNDI B LASHINDWA KUTOA MBABE
Kundi B
katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika lenye timu za Zambia,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Tunisia na Cape Verde limeshindwa
kuibua mbabe baada ya timu zote kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Katika
mchezo wa kwanza wa kundi hilo Zambia iliumana na majirani zake Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo, ambapo Zambia iliweza kujipatia bao la mapema
ikiwa ni katika dakika ya pili lililofungwa na Given Singuluma na kudumu
hadi mapumziko. Hata hivyo Yannick Bolasie aliweza kuisawazishia timu
yake ya DR Congo katika dakika ya 66. Hadi kipenga cha mwisho
kinapulizwa timu zote zilikuwa zimeambulia goli moja na pointi moja.
Timu ya
Tunisia ilivaana na Cape Verde katika mchezo wa pili wa kundi B.
Walikuwa ni Tunisia walioanza kujipatia bao katika dakika ya 70
likifungwa na Ali Moncer. Lakini dakika saba baadaye Cape Verde
ilisawazisha kupitia mkwaju wa penalti uliofungwa na Almeida Ramos.
Mchezo huu nao ulimalizika kwa sare ya 1-1, hivyo kutokuwepo mbabe wa
kundi.
Leo ni mechi za kundi C ambapo Ghana itaonyeshana kazi na Senegal, zikifuatiwa na mchezo kati ya Algeria na Afrika Kusini.
Kundi A
linaongozwa na timu ya Gabon ambayo iliirarua Burkina Faso 2-0 katika
mchezo wa Jumamosi, huku wenyeji Equatorial Guinea wakitoka sare ya 1-1
na Congo.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment