MESSI AFIKISHA HAT TRICK YA 42 BARCA IKIUA 4-0 LA LIGA

BARCELONA
 imejibu mapigo ya Real Madrid iliyoichapa 3-0 Getafe. Barca imepata 
ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Deportivo La Coruna katika La Liga 
usiku huu Uwanja wa Riazor. 
Lionel
 Messi alifunga bao la kwanza kwa Barcelona kwa kichwa maridadi dakika 
ya 10, kisha akafunga la pili zuri, akiwalamba chenga mabeki kabla ya 
kumtungua kipa dakika ya 33. 
Mwanasoka
 huyo wa kimataifa wa Argentina akafikisha hat-trick yake ya 22 katika 
La Liga kwa bao la dakika ya 62, kabla ya beki wa Deportivo, Sidnei 
kujifunga dakika ya 83 kukamilisha pointi tatu dhidi ya timu ya Luis 
Enrique.  
Kikosi
 cha Deportivo La Coruna kilikuwa; Juanfran, Sidnei, Lopo, Luisinho; 
Bergantinos, Dominguez, Medunjanin (Lucas 79); Cuenca, Cavaleiro 
(Rodriguez 46), Riera (Toche 63)
Barcelona;
 Bravo; Jordi Alba, Alves, Pique, Mascherano, Rakitic, Busquets/Bartra 
dk66, Iniesta/Rafinha dk66, Suarez, Messi na Neymar/Pedro dk70.
No comments:
Post a Comment