Wampinga Kabila kuwania urais nchini DRC

Rais wa Drc Congo Joseph Kabila
Polisi 
nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamewafyatulia risasi 
waandamanaji kwenye mji mkuu Kinshasa walio na hasira katika kile 
kinachoonekana kama jitihada za kutaka kuongoza uongozi wa rais Joseph 
Kabila.
Watu 
kadha walitolewa eneo la kati kati mwa mji wakiwa na majeraha ya risasi 
ambapo pia kulitoka makabiliano kwenye chuo kikuu cha mji huo.
Milio ya risasi iliripotiwa katika maandamano mengine katika mji ulio mashariki wa Goma.
Watu 
kadhaa walipatikana na majeruhi ya risasi katikati mwa mji huo huku 
ghasia zengine zikiripotiwa katika katika chuo kimoja kikuu.
Viongozi 
wa upinzani waliitisha maandamano hayo baada ya bunge dogo kuidhinisha 
sheria siku ya jumamosi inayoagiza kufanyika kwa hesabu ya idadi ya watu
 kabla ya uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka ujao.
Wabunge hao wa upinzani wamesema kuwa mpango huo utachelewesha uchaguzi huo ambao umekuwa ukingojwa kwa hamu kwa miaka kadhaa.
Rais 
Joseph Kabila ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka 15 amehudumu miula 
miwili na hawezi kuwania tena urais kulingana na katiba.
Bunge kuu linatarajiwa kuungazia mswada huo wa uchaguzi hii leo.
No comments:
Post a Comment