TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, August 29, 2014

Hatimaye Torres amua kuondoka Chelsea – hii ndio tiku aliyoichagua

IMG_6865.JPG
Fernando Torres amemaliza kipindi kigumu kabisa cha miaka mitatu na nusu kwenye maisha yake ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kukubali kuondoka katika timu hiyo.
Fernando alijiunga na Chelsea mnamo mwaka 2011 January kwa ada ya uhamisho ambayo ilivunja rekodi ya usajili nchini Uingereza – £50m akitokea Liverpool – leo hii imethibitishwa rasmi kwamba mchezaji huyo sasa anajiunga na klabu ya AC Milan ya Italia kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili.
Torres anajiunga na AC Milan kwenda kurithi nafasi ya Mario Balotelli ambaye amejiunga na Liverpool kwa ada ya uhamisho wa £16m.
Torres ameichezea Chelsea mechi 172 na kufanikiwa kuifungia magoli 45 tangu alipotia mguu Stamford Bridge.
Mchezaji huyo anategemewa kwenda Milan kesho tayari kufanyiwa vipiko vya afya

Shinji Kagawa njiani kuondoka Man United – hii ndio klabu anayoenda

1409307188735_wps_2_File_photo_of_Manchester_
Wakati wa utambulisho rasmi wa Angel Di Maria jana, kocha qa man United Louis Van Gaal alithibitishqa kwamba kuna kundi la wachezaji litaondoka mpaka kufikia mwishoni mwa wiki hii.
Leo hii zimetoka taarifa kwamba kiungo wa kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa ni mmoja wa wachezaji wanaondoka kwenye klabu hiyo kabla ya kuisha kwa dirisha la usajili.
Shinji anatarajiwa kujiunga na klabu yake ya zamani ya Borrusia Dortmund kwa ada ya uhamisho wa £8m.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Ujerumani leo hii tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha usajili wake Dortmund.
Kagawa alijiunga na Man United miaka mitatu iliyopita kwa ada ya uhamisho wa £12m.

Alichojibu Ronaldo kuhusu Di Maria kujiunga na Man Utd na kupewa jezi namba 7

Screen Shot 2014-08-29 at 10.19.11 PM
Siku moja baada ya Angel Di Maria kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa klabu ya Manchester United ya England huku akikabidhiwa jezi yenye historia kubwa ndani ya klabu hiyo (namba 7), mwanasoka bora wa ulaya na mchezaji wa zamani wa United, Cristiano Ronaldo amezungumza juu ya Di Maria kwenda Old Trafford pamoja na kupewa jezi namba 7.
Ronaldo ambaye aliondoka Man United mnamo mwaka 2009 kwa ada ya uhamisho ambayo iliweka rekodi ya £80m amesema hana wasiwasi wa Di Maria kufanikiwa ndani ya United.
“Uhamisho huu ni kitu kizuri kwake.” Ronaldo aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Monaco.
“Manchester [United] ni moja ya klabu kubwa duniani, ni sehemu nzuri kwa Di Maria na namtakia kheri na mafanikio,
Di Maria ni mchezaji mzuri sana, anastahili kuichezea United.”
Alipoulizwa juu ya Di Maria kupewa jezi namba 7 aliyokuwa akivaa alipokuwa Man United, Ronaldo alisema: “Nilimwambia, ‘jezi No.7 ina maana kubwa ndani ya United, lakini nadhani ataweza kubeba uzito wa jezi kwa sababu ni mchezaji mzuri sana.”
Di Maria anaweza kuanza kuichezea Man U kesho kwenye mchezo dhidi ya Burnley

ANGELINA JOLIE NA BRAD PITT WAFUNGA NDOA 

BRAD_6a9c1.jpg
Wacheza filamu maarufu wa Marekani, Angelina Jolie na Brad Pitt wamefunga ndoa. Sherehe ndogo ya faragha iliyofanyika nchini Ufaransa, imemaliza miaka na mikaka ya tetesi za vyombo vya habari, ikiwa watafunga ndoa au la, na lini hilo litafanyika. Tayari wana watoto sita, watatu kati yao wakiwa wa kuasili kutoka Cambodia, Vietnam na Ethiopia.(E.L)

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

falcao_ce57b.jpg
Real Madrid wamekamilisha uhamisho wa pauni milioni 20 wa Radamel Falcao, 28, kutoka Monaco (Calciomercato), Arsenal wana matumaini ya kukamilisha uhamisho wa beki Sorkatis Papastathopoulos, 26, kutoka Borussia Dortmund, lakini wamesema hawatalipa pauni milioni 20 (Daily Mirror), boss wa Aston Villa Paul Lambert ametoa dau la pauni milioni 8 kumtaka kiungo wa Manchester United Tom Cleverly, 25, (Daily Telegraph), lakini Lambert huenda wakapata upinzani mkali kutoka Valencia, ambao nao pia wamepanda dau kwa Cleverly (Sky Sports), Danny Welbeck, 23, anajiandaa kuondoka Old Trafford, na akitajwa kwenda Tottenham kwa mkopo (Daily Star), Chelsea wanakaribia kutoa ruhusa kwa Fernando Torres, 30, kwenda Inter Milan (Times), Manchester United wameongeza bidii kumfuatilia kiungo Martin Odegaard, 15, anayechezea Stromsgodset kutoka Norway (Daily Telegraph), Valencia na Juventus wametoa dau la kutaka kumsajili Javier Hernandez, 26, kutoka Manchester United kwa kiasi cha pauni milioni 15 (Guardian), mshambuliaji Demba Ba, 29, alikaribia kujiunga na Arsenal kabla ya kusaini kwenda Besitkas ya Uturuki kutoka Chelsea kwa pauni milioni 8 (Independent), kiungo anayesakwa na Manchester United Arturo Vidal, 27, amekaririwa akisema hataki kuondoka Juventus (Daily Express), kiungo wa zamani wa Arsenal Alex Song, 26, ana matumaini ya kurejea katika Premier League na Liverpool baada ya Barcelona kuonekana kutomtaka (Daily Mirror), kiungo wa PSG Adrien Rabiot ambaye mkataba wake unaisha msimu ujao anasakwa na Roma na Arsenal (Le Parisien). Zimesalia siku tatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa..(E.L)

UGUNDUA WA GESI ASILIA UJAZO WA TRILIONI 50.5 


Na Anitha Jonas – Maelezo
Tanzania imegundua gesi asilia katika maeneo 19 ya mwambao na kina kirefu cha maji baharini ambayo ina ujazo wa trilioni 50.5.
Kati ya maeneo hayo 19 yaligundulika gesi hiyo ,matano yanapatikana katika mwambao na 14 yapo katika kina kirefu cha maji baharini .(Martha Magessa)
Hata hivyo gesi iliyogundulika katika maeneo ya mwambao kama Songo songo na Mnazi Bay kwa sasa inatumika kufua umeme na pia kwa ajili ya matumizi ya viwandani,majumbani na kwenye magari.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro wakati akifungua kongamano la wadau wa mafuta na gesi linalofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa huyo amewataka wadau hao watumie muda wao kutoa maoni yatakayosaidia kuwa Sera ya Mafuta na Gesi asilia itakayowanufaisha watanzania pindi itakapoanza kutumika.
Kandoro ameongeza kuwa ni vema Sera hiyo ikasaidia Serikali kupata mapato yake yatakayotokana na Mafuta na Gesi asilia kwa ajili ya kuleata maendeleo mbalimbali kwa manufaa ya wananchi wake.
"Uandaaji wa sera hii ulipitia marejeo ya nyaraka mbalimbali ikiwemo sera ya petroli za nchi zilizogundua nishati ya mafuta na gesi asilia zikiwemo Uganda,Ghana,Sierra Leone na Pakistani".
Mpaka Oktoba mwaka jana (2013) Serikali ilikuwa imekamilisha sera ya gesi asilia ,hii ni kwa ajili ya kutoa muongozo wa kusimamia na kuendesha biashara ya gesi asilia katika uchakataji,usafirishaji na usambazaji", alisema Kandoro.
Amesema kuwa Sera hiyo itazingatia na kuangalia kwa ukaribu suala la udhibiti wa mazingira ukomo wa uzalishaji wa rasilimali hiyo pale utakapoanza.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Jiolojia kutoka Wizara ya Nishati na Madini Adam Zuberi amesema lengo la sera hiyo ni kuhakikisha rasilimali ya gesi asilia inawanufaisha watanzania wote kwa mapato yatakayopatikana katika maeneo husika kwani asilimia 3 itabaki Halmashauri kwa matumizi ya wananchi.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof. Ibrahim Lipumba ameishauri Serikali kuwa makini katika makubaliano na makampuni yatakayochimba gesi katika mgawanyo wa mapato kama inavyoonyesha katika sera kuwa asilimia 60 ya mapato itapelekwa Serikalini. Pia umakini na uangalifu wa hali ya juu unahitajika kwenye makubaliano hayo.
Mkutano huo wa wa siku moja uliandaliwa na wizara ya Nishati na Madini na kujumuisha wataalam mbalimbali waliobobea katika masuala ya mafuta ,wawakilishi wa ofisi za ubalozi zilizopo nchini ,Vyama vya siasa , viongozi wa dini, Wakuu wa Mikoa na asasi za kiraia .

AJALI YA GARI MBALIZI MKOANI MBEYA LEO HII 

AJARAAAAI1_74646.jpg
Tunaomba radhi kwa kuonyesha picha ya tukio hili, ni taarifa iliyotufikia hivi punde kutoka huko mbalizi Mkoani  Mbeya.(Martha Magessa)

Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita
Eneo hili la ubavuni ndipo eneo ambalo Daladala hiyo iliingia na Kujigonga
 
Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo 
 
Askari wa usalama wa Barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo
Eneo ambalo Daladala hiyo iliyofumuka 

Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea 
Hivi ndivyo Daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyo  Haribika Baada ya ajali hiyo
Mashuhuda wakiwa wamelizunguka daladala hiyo kushuhudia kllichotokea 
 Hapa ndipo eneo ambapo ajali imetokea , Askari wa usalama wa barabarani wakiendelea kufuatilia ajali
hiyo Ilikuwa ni Ajali mbaya
  
Mashuhuda 

Baadhi ya Majeruhi wakiwa wanatolewa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea Hospitali ya Rufaa Mbeya   
WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace  na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia barabarani.
Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi inagawa pia walimtupia lawama dereva wa Fuso ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
 Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako Majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.
Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huklu wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.
Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na Wanaume wanne.
Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio. NA MBEYA YETU BLOG

MKUTANO MAWAZIRI WA MAZINGINGIRA AFRICA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Peter Pinda amefungua mkutano wa Mawaziri wa Afrika wa Mazingira na Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka katika baadhi ya nchi za Afrika jijini Dar-es-salaam leo.(Martha Magessa)
Mkutano huo ambao ufunguzi wake uliongozwa na agenda kuu iliyozungumzia mwongozo wa namna ya kushughulikia changamoto zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabianchi, na ambavyo nchi za Afrika zitakavyoweza kunufaika na rasilimali zinazotolewa na nchi zinazoendelea ili kukabiliana na janga hilo.
Aidha Waziri mkuu Pinda alielezea kuwa mkutano huo pia una umuhimu kwa nchi za bara la Afrika pia utahusisha namna ambavyo serikali za Afrika zinaweza kukabiliana athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabiachi. Pia alisema kuwa mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya mkutano mkubwa wa mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika mjini Newyork Marekani unaotegemewa kufunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Baink Moon.

"Wote tunafahamu kwamba mabadiliko ya Tabianchi yanaathari kubwa kwa dunia nzima ila madhara yake yanatofautiana kutokana na mabara, vizazi, umri, nafasi, matabaka pamoja na kipato" Aliongeza kuwa kutokana na uchumi tegemezi wa nchi nyingi za Afrika nchi hizo zimekuwa zikiathirika zaidi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kiwango kidogo cha kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabianchi na kuwa na uchumi mbovu.
Aliendelea kusema kuwa Afrika na Jamii za kimataifa zinatakiwa kuwa na utashi wa kisiasa katika kuungana kwa pamoja ili kuweza kushirikiana katika kupunguza uzalishaji wa gesi joto pia katika kuhimili na kukabiliana na athari hizo.
Mkutano huo wa Mabadiliko ya tabianchi uliofanyika leo jijini Dar-es-salaam umehusisha baadhi ya Mawaziri wa Mazingira na Mawaziri wa Mambo ya nje ambao ni wajumbe wa kamati ya nchi za Afrika ya Mabadikliko ya Tabianchi.

Wednesday, August 27, 2014

Baada ya wawili kufa kwa Ebola Congo DRC, Mkuu wa mkoa Kigoma ametoa hii

Screen Shot 2014-08-27 at 8.40.36 AM
Taarifa zilizotoka saa kadhaa zilizopita zilionyesha kwamba kati ya Wagonjwa nane waliokutwa na Ebola huko Congo DRC, wawili kati yao wamefariki dunia.
Taarifa hizi zimeendelea kuwashtua na kuwafanya majirani kuzingatia tahadhari ambapo mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa Machibya amesema ‘pamoja na tishio la ugonjwa huu kwamba uko DRC Congo lakini DRC ya mbali sana kule kaskazini wanakopakana na Afrika ya kati na Sudan, tumeanza kuchukua tahadhari kwenye mipaka yetu manake binadamu wanatembea na maingiliano ni makubwa’
‘Kuanzia leo nimemuagiza katibu tawala wa mkoa magari yote yenye uwezo wa kubeba vipaza sauti usiku au jioni watu wamesharudi nyumbani yapite kutangazia Wananchi kwa muda wa siku tatu mfululizo licha ya kuweka vipeperushi’ – Machibya.
John Ndunguru ambae ni katibu tawala wa mkoa amesema ‘Kwenye hospitali zetu wameshatenga chumba maalum kama atatokea mgonjwa yeyote manake inabidi Wagonjwa hawa wawekewe kinga au wigo kwa siku 48, vilevile wizara ya Afya imeahidi kutuletea vifaa vya kutosha hasa vya kinga na dawa mbalimbali, tayari maafisa Afya wako hata uwanja wa ndege kukagua kila anaeingia’

Official: Everton yamsaini Samuel Eto’o lakini kuna kulichomsononesha

IMG_6758.JPG
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya FC Barcelona na Chelsea Samuel Eto’o amekamilisha usajili wa kujiunga na Klabu ya Everton pamoja na kwamba alikuwa akikaribia kujiunga na Liverpool.
Everton amesaini mkataba wa miaka miwili ambapo nahodha huyu wa timu ya taifa ya Cameroon ameripotiwa kusononeshwa na uhamisho wake kwenda Liverpool kufeli wakati akiwa tayari alishafanya mpaka vipimo vya afya.
kwenye sentensi nyingini ni kwamba Eto’o anatarajiwa kuanza kuichezea Everton weekend hii kwa mechi dhidi ya Chelsea ambayo aliitumikia msimu uliopita.

Official: Angel Di Maria ni mchezaji mpya wa Man United na kaivunja hii rekodi

IMG_6749.JPG
Ishu ya usajili wa mchezaji wa kiargentina Angel Di Maria kwenda klabu ya Manchester United kutokea Real Madrid imemalizika rasmi usiku wa August 26 2014 baada ya Manchester United kuthibitisha kukamilisha usajili huo kwa ada ya uhamisho £59.7m.
Hii ada ya uhamisho imeweka rekodi mpya ya uhamisho nchini Uingereza ikivunja rekodi ya £50m ambayo Chelsea waliilipa Liverpool kwa ajili ya usajili wa Fernando Torres.
Di Maria amekabidhiwa jezi namba 7 na amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia Manchester United.
IMG_6752.JPG
IMG_6750.JPG
IMG_6751.JPG
IMG_6748.PNG

Thursday, August 21, 2014

Waandamanaji wataka Nawaz Sharif ajiuzulu 

Waandamanaji wanaotaka waziri mkuu Nawaz Sharif ajiuzulu. Islamabad, Pakistan Aug. 19, 2014.
Waandamanaji wanopinga serikali nje ya bunge la Pakistan, hawaonyeshi ishara yoyote ya kuondoka,hadi pale waziri mkuu Nawaz Sharif atakapojiuzulu, dai ambalo serikali imekataa kwa misingi ya kuwai kinyume na katiba. Wakati huo, huo jeshi lenye nguvu la Pakistan limeonya pande zote kutatua mzozo wao kupitia majadiliano.
Maelfu ya waandamanaji wanopinga serikali wamekuwa katikati ya mji mkuu wa Pakistan kwa karibu wiki moja, katika juhudi za kumshinikiza waziri mkuu Nawaz sharif kujiuzulu.
Wote serikali na viongozi wa maandamano hayo hawaelekei kurudi nyuma, na hivyo kuongeza hofu ya mapambano baina ya polisi na waandamanaji hao kila kuchao.
Mwanasiasa wa upinzani Imran Khan na kiongozi mashuhuri wa kidini Tahir-ul Qadri, wameaanda maandamano ya umma, ingawa si kwa ushirikiano lakini wanamtaka waziri mkuu Sharif kuachia madaraka.
Maandamano hayo dhidi ya serikali yamelazimisha sehemu kubwa ya mji huo kufungwa na kuvuruga maisha ya kila siku pamoja na shughuli za kibiashara.
CHANZO:VOA
(MM)

Israel na Hamas waendelea na mapigano 

Ukanda wa Gaza ukishambuliwa na maroketi
Mgogoro kati ya Israel na Palestina unaendelea. Pande zote mbili zimekuwa zikishambuliana kwa maroketi. Wakati huo huo, Misri inataka mazungumzo ya kuleta amani yaanze tena.
Mgogoro kati ya Israel na Palestina unaendelea. Pande zote mbili zimekuwa zikishambuliana kwa maroketi. Wakati huo huo, Misri inataka mazungumzo ya kuleta amani yaanze tena.
Hali ya wasiwasi imerejea tena kwa wakaazi wa Israel na ukanda wa Gaza. Awali Israel na Hamas walikubaliana kuendeleza muda wa kusitisha mapigano. Lakini makubaliano hayo hayakuheshimiwa. Israel inasema kuwa hapo jana Hamas ilianza kurusha maroketi kuelekea Israel na ndipo Israel ilipojibu mashambulizi.
Wizara ya afya ya Palestina inaripoti vifo vya Wapalestina wasiopungua 10. Wengine 68 wamejeruhiwa. Israel kwa upande wake inasema kuwa ilifanya mashambulizi 60 ya angani. Ni mashambulizi yanayolenga nyumba za viongozi wa Hamas. Lakini sehemu kubwa ya watu wanaokufa ni raia wa kawaida. Bwana mmoja aliyeshuhudia mashambulizi kwa macho anaelezea kusikitishwa kwake na mauaji yanayoendelea. "Familia nzima imeuwawa: Baba, mke wake aliyekuwa na mimba pamoja na watoto wao watatu. Waisraeli wamelenga familia nzima bila kutoa taarifa na bila sababu yoyote."
Katika kisa kingine, watu watatu waliuwawa baada ya nyumba yao kubomolewa na roketi katika ukanda wa Gaza. Nyumba hiyo inaaminiwa kuwa ya kiongozi wa kijeshi wa Hamas, Mohammed Deif. Msemaji mmoja wa Hamas amethibitisha kuwa miongoni mwa waliouwawa walikuwepo mke na mtoto wa Deif. Waziri mmoja wa Israel amenukuliwa akisema kuwa Mohammed Deif anastahili kufa kama vile Osama bin Laden alivyokufa. Waziri huyo aliongezea kuwa Deif ni muuaji na kwamba Israel itatumia kila nafasi itakayojitokeza kujaribu kumuua kiongozi huyo wa Hamas.
Kwa sasa hakuna ishara za mgogoro huu kutulia. Israel imewaandaa maaskari 2,000 wa ziada kwa ajili ya kufanya operesheni za ardhini wakati wowote ule.
Hata mazungumzo ya kuleta amani yaliyokuwa yakiendelea Cairo, Misri yamesitishwa. Wawakilishi wa pande zote mbili wamegoma kuendelea na juhudi za kupata suluhu ya mgogoro. Misri imewaasa Hamas na Israel kurejea katika meza ya mazungumzo, ikisema kuwa inajaribu kushawishi pande zote mbili kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda. Kwa mujibu wa viongozi wa Palestina na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 2,000 wameuwawa tangu mgogoro huu ulipoanza mwezi uliopita.
Mwandishi: Elizabeth Shoo/ap/afp
Mhariri: Saumu Yusuf
CHANZO:DW

RATIBA LIGI KUU BARA 2014/2015 YAANIKWA HADHARANI 

 

DSC_0007-546x291
Kocha mkuu wa Simba sc Patrick Phiri akiongea na wachezaji wake


Kocha mkuu wa Yanga akiongea na msaidizi wake
RATIBA ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 utakaoanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu umeanikwa hadharani na Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF.
Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo katika taarifa yake amesema ratiba hiyo imezingatia michuano ya Chalenji itakayochezwa Novemba, usajili wa dirisha dogo Nov 15- Des 15, ushiriki wa klabu za Azam na Yanga kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa (CL) na Kombe la Shirikisho (CC).(P.T)
Wambura alisema mechi zitachezwa wikiendi ili kuongeza msisimko/kuwapa fursa washabiki wengi zaidi kuhudhuria, na katikati ya wiki imeachwa wazi kwa ajili ya mechi za Kombe la FA (Federation Cup).
Vilevile kutakuwa na mechi Boxing Day na siku ya Mwaka Mpya.
Siku ya ufunguzi zitapigwa mechi saba katika viwanja tofauti nchini ambapo mabingwa watetezi  Azam fc wataanza kutetea ubingwa wao dhidi ya wageni Polisi Morogoro katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es saalam.
Yanga chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo wataanza ugenini katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro dhidi ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar.
Timu mbili zilizopanda ligi kuu msimu huu, Stand United na Ndanda fc zitachuana katika dimba la Kambarage mkoani Shinyanga.
Mgambo JKT watakawakaribisha Kagera Sugar katika dimba la CCM Mkwakwani jinni Tanga.
Ruvu Shooting wataanza kampeni zao katika uwanja wao wa Mabatini uliopo Mlandizi Pwani dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons.
Wagonga nyumbo wa Mbeya City fc wataanza nyumbani katika dimba la CCM Sokoine Mkoani Mbeya dhidi ya JKT Ruvu.
Wekundu wa Msimbazi Simba chini ya kocha Mzambia, Patrick Phiri wao wataanza kampeni za kuusaka ubingwa wa ligi kuu bara septemba 21 dhidi ya Coastal Union uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Raundi ya pili  itacheza septemba 27 na 28 mwaka huu ambapo timu zote zitashuka dimbani.
Septemba 27, wekundu wa Msimbazi Simba watacheza mechi yao ya pili nyumbani dhidi ya Polisi Morogoro.
Mechi nyingine siku hiyo zitakuwa baina ya Mtibwa Sugar dhidi ya Ndanda fc katika uwanja wa Manungu Turiani. Azam watawakaribisha Ruvu Shooting Chamazi, Mbeya City watachuana na Coastal Union uwanja wa Sokoine, wakati Mgambo JKT watakuwa Mkwakwani kuchuana na Stand United.
Raundi ya pili itakamilika septemba 28 ambapo JKT Ruvu watavaana na Kagera Sugar katika uwanja wa Azam Complex.
Mechi nyingine itawakutanisha Yanga sc ya Maximo dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Endelea kufuatilia mtandao huu kwasababu utaendelea kukujuza kuhusu ratiba nzima ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Chanzo:Shaffihdauda.com

Uliipata hii ya Wanafunzi Kenya kupelekwa Mahakamani baada ya kukutwa wamelewa

Screen Shot 2014-08-21 at 12.28.31 PM 
Sio kitu kigeni kuona watu wenye umri zaidi ya miaka 18 wanakunywa Pombe wanalewa na hata pombe hiyo kugharimu maisha yao ila sio kawaida kukutana ama kuona mtoto wa miaka kati ya 14-17 ni mlevi wa kupindukia na mtumiaji pia wa dawa za kulevya.
Ripoti mpya iliyotolewa na Mamlaka ya kudhibiti vileo nchini Kenya (NACADA) inaonyesha kwamba ni watoto zaidi ya MILIONI MOJA nchini humo wenye umri kati ya miaka 14-17 ambao ni watumiaji wakubwa wa pombe na dawa za kulevya.
Kenya Julius Kepkoech amesema mwenyekiti wa NACADA John Mututho ameisema hii wakati alipowatembelea Wanafunzi 16 waliokamatwa wakiwa wamelewa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo sasa wamefikishwa kwenye Mahakama ya Baricho.
Screen Shot 2014-08-21 at 12.30.15 PM 
Hakimu mkuu wa Baricho Hezekiah Keago ameamuru Wanafunzi hao baadhi kurudishwa mikononi mwa wazazi ili kufanyiwa ushauri nasaha lakini pia vilevile Wanafunzi wengine waliobakia kati ya hao wamehukumiwa kwenda jela ya Watoto Muranga.
Ushahidi uliotolewa Mahakamani umeonyesha kwamba hawa Wanafunzi ambao wamekamatwa kwa ishu ya pombe, walihusika kuinywa pia pombe iliyopigwa marufuku nchini Kenya ambayo ina kemikali hatari kwa afya na iliua zaidi ya watu mia moja.

Mfanyakazi wa benki afikishwa mahakamani kwa kuiba pesa za abiria walipotea na Malaysia airline

mala
Mwanamke mmoja mwenye cheo cha juu katika bank kubwa iliyopo Kuala Lumpur Malaysia pamoja na mumewe wameshtakiwa kwa kuiba pesa kutoka katika account za abiria na wafanyakazi wa ndege ya Malaysia iliyopotea kwenye bahari ya hindi.
Pamoja na kushtakiwa huko mtu na mkewe hao waliepuka makosa mengine 16 kati ya makosa hayo yamo wizi,kukaidi amri ya mahakama na makosa mengineyo.
Ofisa huyo Nur Shila Kanan anatuhumiwa kutumia cheo chake vibaya katika benki ya HSBC nchini Malaysia kwa kuiba pesa za abiria walipotea na ndege.
Mwendesha mashtaka aliiambia mahakama moja mjini Kuala Lumpur,Malaysia kwamba wawili hao walifanikiwa kukwapua dola za kimarekani elfu thelathini kutoka katika account tatu tofauti za abiria waliopotea na account moja ni ya mfanyakazi wa shirika hilo la Malaysia airline.

Picha za nyumba mpya ya Justin Bieber yenye night club,gym na movie theater

00
Hivi sasa Justin Bieber anaweza kujiachia kwenye club bila kupigwa picha na mapaparazi kwa sababu nyumba yake mpya ina night club na bar tatu ndani yake.
Japokuwa pesa alizolipa Bieber kumiliki nyumba hii haijawekwa wazi, sifa zake ni kuwa na ukubwa wa square meter 16,000,vyumba vya kulala 10,gym kubwa,bwawa la kuogelea,movie theater yenye screen ya inch 160 na vitu vingine.
Justin Bieber ameshahama kwenye nyumba aliyokuwa amepanga na kuhamia kwenye nyumba hii mpya aliyonunua. Hizi ni picha 10 zikionyesha nyumba hiyo
0
1
2
3
4
5
6
7
8
9

Mtoto wa Jackie Chain akamatwa na gram 100 za bangi

jacki
Jackie Chain ambaye aliwai kuwa balozi wa kampeni za kupinga matumizi ya dawa za kulevya amejikuta kwenye wakati mgumu na kumlazimu kuomba msamaha kwa kwa ajili yake na kwa niaba ya mwanae Jaycee Chain.
Kwenye website yake Jackie Chain ameandika, “Kutokana na swala la mwanangu Jaycee, nimekasilishwa na nimeshtushwa sana. Kama kioo cha jamii najiskia aibu sana, pia kama baba nimeumizwa sana. Mimi na Jaycee kwa pamoja tulazimika kuomba msamaha kwa jamii nzima”.
Jaycee Chain mtoto wa movie star Jackie Chain amekutwa na gram 100 za marijuana kwenye nyumba yake. Jaycee pia ni muigizaji kama baba yake.
ja