TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, August 9, 2014

Iraq:Marekani yaendeleza mashambulizi 

Ndege ya kijeshi ya marekani
Wizara ya ulinzi nchini Marekani imesema kuwa inaendelea kuwashambulia wanamgambo wa taifa la kiislamu kazkazini mwa Iraq.
Taarifa imesema kuwa wanajeshi wa Marekani walitekeleza mashambulizi mengine mawili ya angani ili kuulinda mji wa Irbil ambapo wafanyikazi wa marekani wanapiga kambi.
Mashambulizi hayo yanashirikisha ndege isiyo na rubani pamoja na jengine lililotekelezwa na ndege nne za kijeshi za Marekani katika msafara wa wanamgambo hao na maeneo yao ya kurusha makombora.
Awali katika shambulizi la kwanza tangu Marekani iondoe vikosi vyake nchini Iraq mnamo mwaka 2011,ndege za kijeshi zilishambulia mizinga inayotumiwa na wanamgambo hao kukabiliana na vikosi vya Kikurdi vinavyolinda mji wa Irbil.
Vikosi vya Kikurdi vinasema kuwa wapiganaji hao kwa sasa wameliteka bwawa kubwa nchini Iraq karibu na mji wa Mosul ambalo wanaweza kulitumia kutekeleza mafuriko katika miji kadhaa mbali na kukata usambazaji wa maji na umeme.
Wakati huohuo Hatua ya Marekani kutekeleza mashambulizi nchini Iraq inatokana na wito wa kimataifa kuhusu hatma ya raia wa kikristo pamoja na wale wa Yazidi walio wachache wanaotishiwa na kushambuliwa na wanamgambo wa taifa la kiislamu.
Marekani imeangusha chakula cha msaada kwa makumi ya maelfu ya wakimbizi waliokimbilia hifadhi katika mlima mmoja.Uingereza na Ufaransa pia zimeahidi kuwasidia raia hao.
Umoja wa mataifa pia unaanda njia ya dharura ya kuwafikishia misaada raia hao.
Msemaji wa Umoja wa mataifa anasema kuwa zaidi ya wakimbizi wengine laki mbili wamefika katika mto Tigris katika eneo la Kurdistan nchini Iraq huku maelfu ya wengine wakielekea kazkazini karibu na mpaka wa Uturuki.
Wizara ya haki za kibinaadamu nchini Iraq imesema kuwa kuna hofu kwamba mamia ya wasichana wa Yazidi wametekwa na wanamgambo wa taifa la kiislamu mjini Mosul.

No comments:

Post a Comment