Rais Obama asifu majeshi ya Iraq na kurd
Rais wa Marekani, Barack Obama
Rais wa
Marekani Barack Obama amesema majeshi ya Iraq na yale ya Kikurd yamepiga
hatua kubwa kulitwaa tena bwawa muhimu la Mosul kutoka kwa wapiganaji
wa kiislamu kaskazini mwa Iraq.
Amesema
wamethibitisha kwamba wanauwezo wa kufanya kazi kwa pamoja na
wataendelea kuungwa mkono na majeshi ya Marekani, ambayo tayari
yamefanya mashambulio Zaidi ya anga katika eneo linalokaliwa na
wapiganaji wa kiislamu.
Ripoti zinasema kuwa mapambano katika juhudi za kudhibiti maeneo yanayozunguka bwawa hilo yanaendelea.
Katika
hatua nyingine kundi la himaya ya kiislamu linalofanya mashambulizi
dhidi ya Wakurd limekanusha kwamba wapiganaji wake wamepoteza udhibiti
wa bwawa hilo.
Wakati
huohuo kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amesema jumuia
ya kimataifa itakuwa na haki katika kuchukua hatua dhidi ya wanamgambo
hao .
Papa
Amesema ni halali kuzuia kile alichokiita dhuluma ya kichokozi. Lakini
ametahadharisha kuwa hatua yoyote itakayochukuliwa lazima ifanyiwe
tathmini. kusimamisha na kwamba hakusema. Mwandishi wa BBC MJINI Roma
Italia anasema papa Fransis hajaonesha kuunga mkono mashambulio ya anga
yanayofanywa hivi sasa na Marekani dhidi ya wapiganaji hao wa kiislamu.
No comments:
Post a Comment