WAKILI WA PISTIORIUS ASEMA KESI IMEVURUGWA
Kundi la mawakili
wanaomtetea mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius
wanasema kuwa viongozi wa mashitaka wamevuruga kesi hiyo kwa minajili ya
kumfanya kuwa na makosa
Kwenye taarifa yake ya mwisho wakili
wa Pistorius Barry Roux amesema kuwa bwana Pistorius angefunguliwa
mashitaka ya kuua bila kukusudia bali si ya mauaji baada ya kumpiga
risasi na kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.Bwana Pistorius anasema kuwa alimpiga risi kimakosa akidhani kuwa alikuwa ni jambazi.
Lakini bwana Roux alikiri kwamba Pistorius anapaswa kupatwa na hatia kwa kosa la kutumia silaha yake katika mgahawa.
Wakati kila upande utakapokamilisha kutoa kauli zao ya mwisho jaji ataahirisha kesi hiyo kwa takriban wiki moja kufanya uamuzi.
Mwanariadha huyo amekanusha makosa yake dhidi yake ikiwemo kosa la kutumia silaha yake katika sehemu ya umma pamoja na kumiliki silaha haramu.
bbc
No comments:
Post a Comment