TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, August 16, 2014

PATASHIKA LA LIGI KUU ENGLAND NI LEO

article-2725958-208DCEFD00000578-103_634x823
 Kazi yapamba moto: kocha Louis Van Gaal tayari kuanza maisha mapya Man United
LIGI kuu nchini England inaanza kutimua vumbi leo hii na Louis Van Gaal anaanzisha patashika dhidi ya Swansea City katika uwanja wa Old Trafford.
Kocha huyo wa Kiholanzi mwenye miaka 63 amefanya vizuri katika wiki zake nne za kwanza United, akiiwezesha timu kushinda mechi tano na sare moja katika mechi za maandalizi ya msimu na sasa mashabiki wengi wana hamu ya kuangalia mafanikio yake katika ligi.(P.T)
Swansea ni moja ya timu nane zilizoingia katika rekodi ya kushinda mechi Old Trafford msimu uliopita ambapo Man United ilikuwa inaongozwa na kocha David Moyes aliyefukuzwa mwishoni mwa msimu kutokana na kuvurunda.
Msimu wa 2013/2014, United pia ilikabiliana na Swansea katika mchezo wa ufunguiz wa ligi kuu wakiwa mabingwa watetezi na kushinda mabao 4-1 katika uwanja wa Liberty.
Katika mechi ya leo, Wayne Rooney ataiongoza kwa mara ya kwanza Man United tangu achaguliwe kuwa nahodha jumanne timu ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Valencie.
Kwa upande wa Luke Shaw hataweza kucheza mechi ya leo kwasababu ya kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
1408135236305_wps_3_MANCHESTER_ENGLAND_MAY_11
Watabakiza ndoo?: Manchester City waanza kutetea ubingwa wao waliotwaa msimu uliopita baada ya kuwazidi kete Liverpool
Katika mechi nyingine, Aserne Wenger aliyemaliza ukame wa miaka tisa bila kutwaa kikombe baada ya kuibuka mabingwa wa kombe la FA msimu uliopita na kuanza vizuri msimu kwa kutwaa Ngao ya Hisani baada ya kuifunga Manchester City 3-0 mwishoni mwa wiki iliyopita, ataanza ugenini dhidi ya Crystal Palace isiyokuwa na kocha mkuu baada ya Tony Pulis kutimka kufuatia kutofautiana na wamiliki wa klabu hiyo juu ya sera ya usajili..
Mshambuliaji mpya Alexis Sanchez aliyesajiliwa kwa paundi milioni 30 kutokea Barcelona anatarajia kuwemo katika kikosi cha Asernal kitakachoongozwa na nahodha mpya, Mikel Arteta.
Katika mechi nyingine, Leicester City watacheza mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England tangu mwaka 2004 watakapoikaribisha Everton leo, wakati timu nyingine iliyopanda msimu huu, Queens Park Rangers itachuana na Hull City Uwanja wa Loftus Road.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Manchester City wataanza kutetea taji lao dhidi ya Newcastle United kesho.
Liverpool, wataanza kampeni zao dhidi ya Southampton, ambao wamewauza Adam Lallana, Rickie Lambert na Dejan Lovren kwa Wekundu hao wa Anfield.
Chelsea ya Mreno Jose Mourinho, ikiongozwa na wachezaji wake wapya, Diego Costa na Cesc Fabregas itakabiliana na Burnley iliyopanda msimu huu Jumatatu.
Mechi nyingine; Stoke City na Aston Villa, West Bromwich Albion na Sunderland na West Ham United dhidi ya Tottenham Hotspur, wakati kesho Liverpool v Southampton, Newcastle United v Manchester City na keshokutwa Burnley v Chelsea.

No comments:

Post a Comment