MKUTANO MAWAZIRI WA MAZINGINGIRA AFRICA
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Peter Pinda
amefungua mkutano wa Mawaziri wa Afrika wa Mazingira na Mawaziri wa
Mambo ya nje kutoka katika baadhi ya nchi za Afrika jijini Dar-es-salaam
leo.(Martha Magessa)
Mkutano
huo ambao ufunguzi wake uliongozwa na agenda kuu iliyozungumzia mwongozo
wa namna ya kushughulikia changamoto zitokanazo na athari za mabadiliko
ya tabianchi, na ambavyo nchi za Afrika zitakavyoweza kunufaika na
rasilimali zinazotolewa na nchi zinazoendelea ili kukabiliana na janga
hilo.
Aidha
Waziri mkuu Pinda alielezea kuwa mkutano huo pia una umuhimu kwa nchi za
bara la Afrika pia utahusisha namna ambavyo serikali za Afrika zinaweza
kukabiliana athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabiachi. Pia alisema
kuwa mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya mkutano mkubwa wa mabadiliko
ya Tabianchi utakaofanyika mjini Newyork Marekani unaotegemewa
kufunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Baink Moon.
"Wote tunafahamu kwamba mabadiliko ya Tabianchi yanaathari kubwa kwa dunia nzima ila madhara yake yanatofautiana kutokana na mabara, vizazi, umri, nafasi, matabaka pamoja na kipato" Aliongeza kuwa kutokana na uchumi tegemezi wa nchi nyingi za Afrika nchi hizo zimekuwa zikiathirika zaidi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kiwango kidogo cha kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabianchi na kuwa na uchumi mbovu.
Aliendelea
kusema kuwa Afrika na Jamii za kimataifa zinatakiwa kuwa na utashi wa
kisiasa katika kuungana kwa pamoja ili kuweza kushirikiana katika
kupunguza uzalishaji wa gesi joto pia katika kuhimili na kukabiliana na
athari hizo.
Mkutano
huo wa Mabadiliko ya tabianchi uliofanyika leo jijini Dar-es-salaam
umehusisha baadhi ya Mawaziri wa Mazingira na Mawaziri wa Mambo ya nje
ambao ni wajumbe wa kamati ya nchi za Afrika ya Mabadikliko ya
Tabianchi.
No comments:
Post a Comment