Waandamanaji wataka Nawaz Sharif ajiuzulu
Waandamanaji
wanopinga serikali nje ya bunge la Pakistan, hawaonyeshi ishara yoyote
ya kuondoka,hadi pale waziri mkuu Nawaz Sharif atakapojiuzulu, dai
ambalo serikali imekataa kwa misingi ya kuwai kinyume na katiba. Wakati
huo, huo jeshi lenye nguvu la Pakistan limeonya pande zote kutatua mzozo
wao kupitia majadiliano.
Maelfu ya
waandamanaji wanopinga serikali wamekuwa katikati ya mji mkuu wa
Pakistan kwa karibu wiki moja, katika juhudi za kumshinikiza waziri mkuu
Nawaz sharif kujiuzulu.
Wote
serikali na viongozi wa maandamano hayo hawaelekei kurudi nyuma, na
hivyo kuongeza hofu ya mapambano baina ya polisi na waandamanaji hao
kila kuchao.
Mwanasiasa
wa upinzani Imran Khan na kiongozi mashuhuri wa kidini Tahir-ul Qadri,
wameaanda maandamano ya umma, ingawa si kwa ushirikiano lakini wanamtaka
waziri mkuu Sharif kuachia madaraka.
Maandamano
hayo dhidi ya serikali yamelazimisha sehemu kubwa ya mji huo kufungwa
na kuvuruga maisha ya kila siku pamoja na shughuli za kibiashara.
CHANZO:VOA
(MM)
No comments:
Post a Comment