Nakukutanisha na mapacha wasio na birthday moja
Kwa kawaida mapacha wanazaliwa siku moja wakiwa wametofautiana muda mfupi sana na mara nyingi huwa inakuwa ni sekunde au dakika toka wakati anapozaliwa mmoja mpaka wakati anakozaliwa mwingine na hii ni kwa sababu kibaiolojia haiwezekani kwa watoto wawili kutoka tumboni kwa wakati mmoja.Lakini Uingereza imeweka rekodi hii ya kuwa na watoto mapacha ambao siku zao za kuzaliwa ziko kwenye tarehe mbili tofauti yaani kama mmoja amezaliwa tarehe 1 mwingine amezaliwa tarehe 2.
Huko Bolton watoto Scarlett na Robbyn wameweka rekodi hii baada ya mama yao kujifungua watoto wawili kwenye tarehe mbili tofauti, ilianza kama utani wakati ambapo mama huyo aliingia kwenye maumivu ya uchungu wa kuzaa saa chache kabla ya kuingia kwa siku mpya ambayo kwa mahesabu ya kidunia huanza saa sita usiku.
Kabla ya kufika kwa saa sita kamili usiku majira kama ya 5 na dakika 45 usiku mama huyo alijifungua mtoto mmoja huku akingojea kujifungua mwingine kwani alifahamu fika amebeba mapacha.
Mtoto mwingine alikuja kuzaliwa dakika 18 baada ya saa sita usiku kupita na hivyo kufanya ionekane kuwa watoto mapacha Robyn na Scarlett wamezaliwa kwenye tarehe za siku mbili tofauti mmoja akiwa amezaliwa saa tano usiku kabla ya siku mpya kuanza na mwingine akiwa amezaliwa baada ya saa sita usiku saa chache baada ya siku mpya kuanza.
No comments:
Post a Comment