Thierry Henry kurudi Arsenal?

Nyota wa zamani wa Arsenal Thierry Henry ameiaga timu yake ya New York Red Bulls aliyokuwa anaichezea baada ya mkataba wake kuisha .
Henry ameichezea Red Bulls kwa muda wa miaka minne na nusu na inadhaniwa kuwa huenda akatangaza kustaafu soka baada ya kuwa kwenye mchezo huo kwa karibu miaka 20 .
Henry ambaye katika ubora wake aliwahi kuzichezea timu za As Monaco , Juventus , Arsenal na Fc Barcelona ukiachilia mbali timu ya taifa ya Ufaransa alinukuliwa akisema kuwa angependa kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Arsenal ambako inaaminika kuwa atajiunga na benchi la ufundi chini ya kocha wake wa zamani Arsene Wenger .

Moja ya ishara zilizowapa watu sababu ya kuamini kuwa huenda kuna mpango wa nyota huyo kurejea Arsenal ni kitendo chake cha kubadili picha ya ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Facebook ambapo alitoa picha inayomuonyesha akwia amevalia jezi ya New York Red Bulls na kuweka picha ya uwanja wa nyumbani wa Arsenal The Emirates Stadium .

Timeline ya ukurasa rasmi wa facebook wa Thiery Henry ikionyesha uwanja wa Emirates unaotumiwa na Arsenal .
Kocha wa klabu ya Girondins Bordeaux Willy Sagnol ambaye aliwahi kucheza na Henry kwenye timu ya taifa ya Ufaransa amemkaribisha nyota huyo kujiunga naye kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo inayoshiriki ligi ya Ufaransa ofa ambayo Henry bado hajakubali au kutoa tamko la kuikataa .

Henry alijiunga na New York Red Bulls wakati mkataba wake na Fc Barcelona ulipomalizika na amekuwa moja kati ya wachezaji walisaidia kupandisha umaarufu kwenye ligi ya Marekani maarufu kama MLS .
No comments:
Post a Comment