WAKATI SSERENKUMA AKITUA, SIMBA KUSAINI BEKI WA KATI KUSUKA SIMBA MPYA
Na Baraka Mbolembole,
Wakati
kiungo raia wa Uganda, Danny Sserenkuma akitaraji kutua nchini Jumatano
hii kujiunga na Simba SC, Suleimani Matola ambaye ni kocha msaidizi wa
mabingwa hao mara 19 wa kihistoria wa Tanzania Bara amesema kuwa timu
yake ilimuhitaji zaidi kiungo Mkenya, Paul Kiongera lakini kutokuwa na
uhakika wa urejeo wake uwanjani wanalazimika kuweka mbinu zao kwa
Sserenkuma wakati huu wakihitaji kurudisha ubingwa wa ligi ambao mara ya
mwisho waliutwaa msimu wa 2011/12.
Matola
amesema kuwa Simba inatakiwa kumsajili mlinzi wa kati licha ya
kumpandisha kutoka kikosi pili kijana,, Hassan . Simba ilihitaji
kiungo-mbunifu katika eneo lake la mbele, Sserenkuma mwenye kasi,
chenga, mpigaji hodari wa mipira iliyokufa, mfungaji makini, ni mchezaji
mwenye maarifa mengi binafsi ambaye wakati mwingine anaweza kuibeba
timu nzima katika mabega yake na kuipatia matokeo.(P.T)
Usajili
wa dirisha kubwa ulifanywa kwa pupa, haukukidhi mahitaji muhimu ya
nafasi lakini hilo linaweza ‘ kusahihishwa’ vizuri na usajili huu mdogo,
na Matola amekiri wazi kuwa Sserenkuma ni chaguo ambalo Simba
walilitaka. Uwepo wa Emmanuel Okwi, Amis Tambwe na Sserenkuma unaileta ‘
Simba Mpya katika msimu uleule’. Ushindi mara moja katika michezo saba
ya mwanzo msimu huu ni matokeo mabaya.
Lakini
faida kubwa kwa Simba ni kwamba timu za juu nazo hazikuwa na matokeo
bora kuliko. Simba wapo nyuma kwa pointi tano dhidi ya viongozi Mtibwa
Sugar. Kufunga mabao ilikuwa tatizo, lakini pia safu ya ulinzi ilikuwa
na ‘ matobo’ ambayo yameruhusu mabao sita. Ni mechi mbili tu ambazo
Simba haijaruhusu bao ( Yanga SC 0-0 Simba SC, Simba 1-0 Ruvu Shooting),
wamefunga mabao saba katika michezo saba, ila hawajafunga katika mchezo
mmoja tu.
Hii ni
dalili na ubora wa timu, lakini katika ligi yenye mabadiliko ya kimbinu
na ufundi, wachezaji kama Sserenkuma ni wa lazima kwa timu yenye malengo
makubwa. Kuelekea mchezo wa hisani ‘ Nani Mtani Jembe-2′ kati ya Simba
na Yanga wiki ijayo, Simba hawatajali sana matokeo, ila hawatapenda
kufungwa na mahasimu wao, watatazama vizuri uwiano wa kiuchezaji kati ya
idara na idara, kiucheza
TAMBWE, OKWI, SSERENKUMA,
Ni mfumo
gani ambao utawapanga ‘ nyota watatu wa kimataifa’ katika safu ya
mashambulizi?. Nani ambaye atafurahi kuona Tambwe akizungukwa na Okwi
akitokea upande wa kushoto, Sserenkuma akitokea upande wa kulia na guu
lake la kushoto?. Wakati wa kilele cha mafanikio ya FC Barcelona barani
Ulaya, David Villa, Pedro Rodriguez na Leo Messi walitengeneza utatu wa
hatari katika safu ya mashambulizi, hii ndiyo safu ya mashambulizi
iliyomtetemesha, Sir Alex Ferguson pale Wembley, Mei, 2011 katika
fainali ya mabingwa ulaya.
Katikati
ya uwanja walikuwa na ‘ pass-masters, Xavi Hernandez, Andres Iniesta
ambao walisaidiwa katika ukabaji na kijana mahiri katika upokonyaji wa
mipira na kuanzisha pasi sahihi kwa wenzake, Sergio Busquets. Kila mtu
wa soka anakumbuka kuhusu ubora wa ‘ Barca ya Pep Guardiola’ katika
mfumo wa 4-3-3. Je, Patrick Phiri anaweza ku-copy na ku-paste na
kuifanya Simba kucheza huru na kupata matokeo katika mfumo ambao
ulimpatia mafanikio makubwa Pep?.
Phiri
anaweza sababu alishafanikiwa kwa matumizi Ya mfumo huo. Ujanja wa Okwi
katika ufungaji na utengenezaji wa nafasi za mabao kwa wenzake. Okwi
amefunga mabao matatu msimu huu, Tambwe amefunga bao moja, wakati Danny
anatua akiwa na tuzo ya ufungaji bora kutoka KPL. Itashangaza kama Simba
wataendelea kufunga kwa ku-bahatisha mara baada ya ujio wa Sserenkuma.
ndiyo
kwenye soka, majina makubwa si kigezo cha ushindi, lakini mafanikio
binafsi ya Tambwe, Okwi na Sserenkuma yanawatambulisha kama wachezaji
bora kutoka nje ya nchi ambao wapo katika ligi kuu ya Tanzania Bara.
Utulivu, uvumilivu, u-tayari, uwajibikaji ni baadhi ya mambo muhimu
ambayo wachezaji wanatakiwa kuwa nayo, ata mashabiki, wanachama na
viongozi wa klabu.
Kilicho
muhimu zaidi ni mbinu za mwalimu na namna wachezaji wake watakavyoweza
kuchukua mafunzo kutoka katika viwanja vya mazoezi na kwenda nayo katika
michezo rasmi huku wakiwafanya kwa kiwango kisichopungua asilimia
70-65.
Chanzo:http://shaffihdauda.co.tz/
No comments:
Post a Comment