Ule ugeni kutoka Himaya ya Kifalme Uingereza umekutana na mastaa wengine Marekani, picha zipo hapa
Vyombo
 vikubwa vya habari Duniani pamoja na mitandao ya kijamii viliripoti 
kuhusu ziara ya siku tatu inayofanywa na mjukuu wa Malkia 
Elizabeth, Prince William na mke wake Kate Middleton huko Marekani na 
tukapewa taarifa siku ya jana pia kwamba ugeni huo ulipata nafasi 
kuingia ndani ya Ikulu ya Marekani kwa mara ya kwanza na Prince akafanya
 mazungumzo na Rais Obama.
Habari kubwa kwa sasa ni kuhusiana na 
wawili hao siku ya jana kuhudhuria mechi ya Basketball na kuushuhudia 
ushindi wa Cleveland Cavaliers dhidi ya Brooklyn Nets na kupata nafasi 
ya kukutana na staa wa Basketball LeBron James, Jay Z pamoja na Beyonce.
Walipata nafasi ya kupiga stori kidogo na mastaa hao baada ya mechi hiyo kuisha.

Prince
 William, Kate, Jay Z na Beyonce wakisalimiana baada ya kukutana katika 
Ukumbi wa Barclays Centre ilipokuwa ikichezwa mechi ya Basketball kati 
ya Cleveland Cavaliers na Brooklyn Nets jana Desemba 09.




No comments:
Post a Comment