Ndege ya KDF yaanguka Somalia
Ndege ya jeshi la KDF nchini Kenya imeanguka katika eneo la Kismayu nchini Somali.
Ndege
hiyo ilianguka siku ya Alhamisi mwendo wa saa tisa na robo ilipokuwa
ikirudi Kenya baada ya kutekeleza mashambulizi katika eneo la Jamaame
kusini mwa Somalia.
Kulingana
na msemaji wa Jeshi kanali david Obonyo: ''Ndege ya KDF iliokuwa
ikirudi nchini Kenya baada ya kufanya mashambulizi katika eneo la
Jamaame kusini mwa Somali,ilikumbwa na matatizo ya kiufundi na kuanguka
katika eneo la Kismayu .
Kanali Obonyo hata hivyo hakusema iwapo kulikuwa na majeruhi yoyote.
Jeshi la
Kenya limesema kuwa ndege hiyo ilianguka kutokana na hitilafu za
kimitambo baada ya kufanya oparesheni katika eneo la Jamaane Kusini mwa
Somalia.
Hata
hivyo baadhi ya mitandaoa iliyohusishwa na kundi la AL shabaab
imechapisha habari kuwa AL shabaab wamedai kuwa ndio waliodungua ndege
hiyo mwendo wa saa tisa Alasiri, Afrika Mashariki.
Msemaji
wa kiksoi cha kivita cha Al shabaab Sheikh Abdi Azizi Abu Musab
amenukuliwa akisema kuwa walishambulia ndege hiyo kwa kombora baada ya
kulipua kijiji cha Bulaguduud.
Kwa
mujibu wa mwandishi wa BBC wa idhaa ya kisomali, ni vigumu kwa Al
Shabaab kufanya shambulio kama hilo katika mji wa Kismayu kwa kuwa eneo
hilo zima limefurika vikosi vya usalama vya AMISOM.
Mnamo
mwaka wa 2012, majeshi ya Kenya yaliuteka mji wa bandari wa Kismayu,
unaotazamiwa kuwa mji muhimu sana wa kiuchumi katika eneo zima la
Somalia kutoka kwa wanamgombo hao wa Al shabaab.CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment