Pale ambapo operator anajikuta akiweka picha za utupu katika bango uwanjani.
Ajali popote, huyu jamaa amepata ajali kazini tena huenda katika mazingira ambayo hakuwahi kutarajia.
Kutokana na sheria kali za China, hii haikuwa makusudi lakini kwa sababu tayari kashafanya kosa anastahili hukumu.
Tumezoea kuona mabango ya kisasa 
katikati ya Miji kama Dar ambayo yanakuwa yanaonyesha picha kama Tv 
ambapo picha zinazoonekana kuwa zinabadilika badilika.
Nje ya Uwanja wa Maryland, Langzhou China
 jamaa anayehusika kuoperate bango moja amejikuta akiwa na hatia ya 
kukaa jela kwa siku 15 pamoja na na kulipa faini ya kiasi cha Yuan 3000 
za China zaidi ya Dola 484 kwa kosa la kuweka picha za wasichana wakiwa 
tupu kwenye bango lililopo nje ya uwanja huo.
Japo walinzi waliwahi kuchomoa waya wa 
umeme kulizima bango hilo haikusaidia, watu walioshuhudia picha hizo 
zikionekana kwa  sekunde 12 walirekodi video na picha ambazo walianza 
kushare kupitia mitandao ya kijamii.
Mhandisi wa Kampuni inayohusika na kuweka mabango hayo naye pia amekamatwa japo hukumu yake bado haijafahamika.

No comments:
Post a Comment