TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, December 5, 2014

Hollande ziarani Kazakhstan 

Rais wa Ufaransa, François Hollande, amejielekeza KazakhstanIjumaa Desemba 5, ili kuimarisha uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili.
Rais wa Ufaransa, François Hollande, amejielekeza KazakhstanIjumaa Desemba 5, ili kuimarisha uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili.
Na RFI
Ni ziara ya tatu ya rais wa Ufaransa nchini Kazakhstan tangu kutangazwa uhuru wa taifa hilo mwaka 1991. François Mitterrand na Nicolas Sarkozy marais wa zamani wa Ufaransa walifanya ziara ya kikazi nchi Kazakhstan kabla ya François Hollande.
Rais Hollande amewasili nchini Kazakhstan Ijumaa Desemba 5 mapema asubuhi, kwa ziara ya saa 48, ambapo lengo ni kuimarisha uchumi na biashara kati ya Ufaransa na nchi hiyo yenye nguvu katika ukanda wa Asia ya Kati.(P.T)
Kazakhstan ni nchi tajiri kutokana na rasilimali za madini hususan madini ya uranium, kwani ni ya kwanza kwa kuzalisha madini hayo ulimwenguni. Kazakhstan inazungukwa na rasilimali kama chuma, makaa ya mawe, dhahabu, fedha na kadhalika. Fedha zinazotokana na mauzo ya dhahabu nyeusi nje ya nchi inawakilisha peke yake zaidi ya nusu ya mapato ya serikaliya Kazakhstan.
Kazakhstan ni nchi jirani ya mataifa yenye nguvu ambayo ni Urusi na China. Makampuni mengi barani Ulaya yameendelea baada ya nchi zao kuanzisha bishashara na Kazakhstan.
Kwa sasa Ufaransa inachukua nafasi ya tanu katika masuala ya biashara, huku Italia ikiongoza kwa kuchukua nafasi ya kwanza.
Ufaransa inawakilishwa nchini Kazakhstan na kampuni ya mafuta Total, ambayo ni mshirika wa kampuni ya gesi ya Kashagan, aidha Areva, kampuni inayoendesha shughuli zake katika migodi ya Uranium kusini mwa nchi. Kazakhstan ni nchi ya kwanza kwa kuitolea Ufaransa kiwango kikubwa cha uranium.
Hata hivyo Ufaransa inaiuzia Kazakhstan helikopta na silaha nyingi. Ziara hiyo ya rais Hollande nchini Kazakhstan ina manufaa makubwa kwa uchumi wa Ufaransa. Rais Hollande ameshirikiana katika ziara hiyo na ujumbe mkubwa wa matajiri wa makampuni makubwa nchini Ufaransa kama EDF, GDF, Veolia, Airbus, Peugeot pamoja na Vinci.
Hayo yakijiri Kazakhstan imekua ikinyooshewa kidole na mashirika ya haki za binadamu kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.

No comments:

Post a Comment