Matokeo ya UEFA Champions League yapo hapa

Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imeendelea usiku huu ikiwa kwenye mzunguko wake wa mwisho wa hatua ya makundi .
Katika michezo iliyopigwa hii leo timu ya Arsenal toka England ilifanikiwa kushinda kwenye mchezo wake dhidi ya Galatasaray ya Uturuki kwa matokeo ya 2-4 katika mchezo uliopigwa huko Istanbul.
Arsenal ilifunga mabao yake kupitia kwa 
Aaron Ramsey na mshambuliaji raia wa Ujerumani Lukas Podolski ambapo 
kila mmoja alifunga mabao mawili .
Katika mchezo mwingine wa kundi D 
wawakilishi toka Ujerumani, Borrusia Dortmund walibanwa mbavu 
wakilazimishwa sare ya 1-1 katika mchezo dhidi ya Anderlecht ya 
Ubelgiji.
Matokeo haya yanamaanisha kuwa timu za 
Arsenal na Borrusia Dortmund zimefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ambapo
 Dortmund wamefuzu kama washindi huku Arsenal wakishika nafasi ya pili .
Katika michezo mingine iliyochezwa usiku
 huu Real Madrid walifanikiwa kushinda mchezo wao wa 19 mfululizo katika
 mashindano yote wakiwafunga Ludogorets toka Bulgaria 4-0 .

Wafungaji wa Real kwenye mchezo huo walikuwa Cristiano Ronaldo , Gareth Bale , Alvaro Arbeloa na Alvaro Medran .
Ushindi huu umewafanya Real wafuzu hatua
 ya 16 bora kwa kishindo wakiwa wamekusanya pointi 18 baada ya kushinda 
michezo yote 6 ya kundi lao .
Liverpool ambayo ilikuwa nyumbani 
ikicheza na Fc Basle iliambulia sare ya 1-1 matokeo ambayo yalikuwa na 
faida kwa wapinzani wao ambao wanaungana na Real Madrid kufuzu hatua ya 
kwanza ya mtoano.
Katika michezo mingine Juventus na Atletico Madrid walitoka sare ya 
bila kufungana , Olympiakos wakawafunga Malmo 4-2 , Benfica na Bayer 
Leverkusen nazo zikatoka sare ya 0-0 , huku As Monaco ikishinda dhidi ya
 Zenith St Petersburg kwa matokeo ya 2-0 .Kwa matokeo haya timu za Juventus , Atletico Madrid , Monaco na Bayer Leverkusen zinaungana na Arsenal , Dortmund , Real Madrid na Fc Basel kufuzu hatua ya 16 bora .



No comments:
Post a Comment