Alichokiandika Bill Cosby kuhusu shutuma za kubaka zinazomkabili

Mzee Bill Cosby, mchekeshaji maarufu Marekani ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ubakaji ambapo jumla ya kesi 20 kwa mara ya kwanza amejitokeza na kuzungumzia shutuma zinazomkabili.
Watu wengi walionekana kumlaani Cosby 
kuhusiana na shutuma zinazomkabili lakini wapo wachache ambao walisimama
 upande tofauti ambapo ndiyo waliompa nguvu ya kutweet akiwashukuru kwa 
kuonyesha kumpa moyo.
Cosby alitweet akiwashukuru Whoopi Goldberg na Jill Scott
 ambao walieleza kwa nyakati tofauti namna ambavyo hawakupendezwa na 
kitendo cha vyombo vya habari kueneza kashfa za ubakaji juu ya Cosby.
Cosby hakuwahi kuzungumza hadharani 
kujibu chochote kuhusiana na shutuma hizo za ubakaji, japo shutuma 
zinazozungumziwa sasa zinafanya idadi ya wanawake ambao wamewahi 
kuripoti kuhusu kufanyiwa hivyo kufikia 20.
No comments:
Post a Comment