Yule mama aliyejiuzulu kwa kukosoa mavazi ya watoto wa Obama kumbe bado anafuatiliwa?
Moja
ya story ambazo zilichukua uzito wa juu katika vyombo vya habari wiki
iliyopita ilikuwa ni kitendo cha yule mama mfanyakazi wa Chama cha
Republican Marekani, Elizabeth Lauten ambaye alikuwa kitengo cha
Mawasiliano kukosoa mavazi ya watoto wa Obama bado ni story inayoendelea
kuzungumziwa.
Mama huyo aliwaponda Sasha na Malia
kuwa wamekosa ustaarabu kutokana na kuvalia sketi fupi katika hafla ya
chakula katika Ikulu ya White House, pia alisema kuwa watoto hao ni kama
hawakuwa na nyuso za furaha kuwa katika hafla hiyo, ambapo baada ya
kushambuliwa na watu kwenye ukurasa wake wa Facebook aliomba radhi, na
baadaye akajiuzulu.
Leo ni siku ya nne tangu amejiuzulu
lakini story ni kwamba bado ameendelea kufuatiliwa na vyombo habari,
huku wengine wakipiga kambi nyumbani kwa wazazi wake kuchunguza vitu
mbalimbali ikiwemo rekodi ya maisha yake ya utotoni ambapo watu kwenye
mitandao ya kijamii wamekosoa kwa kusema hiyo haikuwa ‘big deal’ ya
kufanya vyombo vya habari kumfuatilia kiasi hicho.
No comments:
Post a Comment