TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, December 1, 2014

Siku ya kupiga vita dhidi ya ukimwi duniani 

Bango linalotahadharisha tatizo la Ukimwi nchini Afrika Kusini na wito kwa kupambana dhidi ya ugonjwa huo.
Bango linalotahadharisha tatizo la Ukimwi nchini Afrika Kusini na wito kwa kupambana dhidi ya ugonjwa huo.
Na RFI
Vita dhidi ya Ebola visipelekei kusahau kupambana dhidi magonjwa yanayoathiri afya ya watu kama ukimwi. Kufuatia siku ya kupiga vita dhidi ya ukimwi duniani, ripoti kadhaa zinaonyesha takwimu za kutia moyo, ikiwa ni pamoja na ile ya milioni 15, kwa mfano.
Hii ni idadi ya watu ambao wanaweza kunufaika kutokana na matibabu katika mwaka 2015. Hata hivyo, vita dhidi ya VVU viko mbali kufaulu.(P.T)
Iwapo takwimu zinaonyesha maendeleo ya kweli katika mapambano dhidi ya Ukimwi, takwimu hizo huficha mara nyingi ukweli wa hali ya mambo. Maambukizi mapya, ambayo ni takwimu muhimu kwa kupungua kwa Ugonjwa huo zimepungua kwa theluthi tatu tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000, lakini pia kukosekana kwa usawa kunaonekana kuko juu. Katika nchi nyingi kusini mwa Sahara barani Afrika, lengo la kupunguza idadi ya maambukizi haliwezi kukamilika.
Uchunguzi wa mwaka huu unaonyesha kuwa dunia imefikia hatua ya mageuzi katika kufikia mwanzo wa mwisho wa Ukimwi. Iwapo mafanikio makubwa yamewezesha nchi 26 kupunguza nusu ya maambukizi yao mapya, wanapaswa kujua kwamba kwa upande mwingine, watu waliotengwa au kubaguliwa, wameendelea kushuhudia ongezeko la maambukizi.
Ni vema kuelewa kwamba huduma bora pamoja na kufanya vipimo mara kwa mara bila kusahau kuendelea kupata tiba vinapaswa kupewa kipaumbele Kaskazini na Kusini ili kukomesha maambukizi mapya kwa lengo la kupiga vita Ukimwi. Zoezi la kuhamasisha na kutoa taarifa kwa vijana wanaoishi kusini mwa Sahara barani Afrika linabakia kuwa suala muhimu katika kupambana dhidi ya Ukimwi.
Tangu kuzuka kwa virusi vya Ebola vinavyoendelea kushuhudiwa Afrika Magharibi sekta ya Afya imeendelea kukabiliana na mdororo wa mfumo wa matibabu , kwa sababu hata kama upatikanaji wa huduma bado unawezekana, wafanyakazi wa afya kwa kiasi kikubwa wameathirika. Mbio dhidi ya muda zilianza ili janga la Ukimwi lisiendelei kupata nafasi katika mataifa hayo.

No comments:

Post a Comment