Sing'atuki ng'o:Mugabe
Rais Robert Mugabe awalaumu baadhi ya wapinzani wake ndani ya chama cha ZANU PF kwa kupanga kumuondoa mamlakani.
Rais wa
Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu baadhi ya watu ndani ya chama chake
tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'oa madarakani.
Akizungumza
katika kongamano la chama hicho, Mugabe amesema amebaini kuwepo
majaribio ya kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi, lakini
akasisitiza wajumbe hawawezi kupokea hongo.
Mugabe
ameahidi kupambana na rushwa ndani ya chama na kukabiliana na maafisa wa
chama hicho ambao kazi yao ni kutoa hongo na kupokea rushwa.BBC
Wanachama wengi wa chama hicho wangali ni wafuasi sugu wa Rais Mugabe
Hasira ya
Mugabe ilionekana kufuatia madai ya njama ya kutaka kumuua yanayodaiwa
kuandaliwa na naibu wake Joyce Mujuru. Hata hivyo Mujuru alikanusha
madai hayo ambayo yamekuwa yakimuandamana.
Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa.
Kadhalika Mugabe amesema Mujuru ni mwizi anayepanga kumuondoa mamlakani kwa kushirikiana na maafisa wengine wa chama.
Maelfu ya wajumbe wa chama walihudhuria kongamano hilo mjini Harare
Chama
tawala cha Zimbabwe kinakumbwa na vita vya ndani kwa ndani kuhusiana na
nani atarithi nafasi ya Mugabe ambaye ana miaka 91 na ambaye ameongoza
tangu uhuru wa taifa hilo.
Hata hivyo amekanusha madai ya kwamba anataka kujiuzuru na kusema kuwa huo ni upuuzi.
Hivi
karibuni afisa mwingine mkuu wa chama tawala, Robert Gumbo aliiambia BBC
kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 90 amegeuza chama tawala na
kukifanya kama mali yake binafsi.
Bi Joyce Mujuru amedaiwa kupanga njama ya kumuua Mugabe ili achukue mamlaka kutokla kwake.
Gumbo alisema lengo kuu la Mugabe ilikuwa kuendeleza uongozi wa chama kwa niaba ya mke wake Grace.
Bi Mujuru
ambaye amekanusha madai hayo alionekana kama mtu ambaye anechukua
usukani wa chama kutoka kwa Mugabe ambaye walipigania naye uhuru wa nchi
hiyo kutoka mikononi mwa watwala wazungu.
No comments:
Post a Comment