Urusi lazima ijitegemee:Putin
Rais
Vladimir Putin amewaonya wananchi wa Urusi kuwa watakabiliwa na wakati
mgumu siku za usoni na kuwataka kujitegemea, amesema katika hotuba yake
kwa taifa akilihutubia bunge.
Urusi
imeathirika kwa kiasi kikubwa kiuchumi kutokana na kushuka kwa bei za
mafuta na vikwazo kutoka nchi za magharibi vilivyowekwa dhidi ya Urusi
kwa kujiingiza katika mgogoro wa nchi jirani ya Ukraine.
Sarafu ya
Urusi ya rouble, ikiwa ishara ya utulivu chini ya utawala wa Bwana
Putin, ilipata anguko kubwa la siku moja, Jumatatu kuwahi kushuhudiwa
tangu mwaka 1998.
Serikali imeonya kuwa Urusi itaingia katika kipindi cha mtuamo mwaka ujao.
Akizungumza
na mabaraza yote mawili ya bunge la Kremlin, Bwana Putin pia
amezishutumu serikali za magharibi kutaka kuiwekea Urusi vikwazo vipya.
Ameeleza kuwa hajutii kulitwaa jimbo la Ukraine la Crimea, akisema eneo hilo lina maana kubwa kwa Urusi.
Amesisitiza
kuwa mkasa huo kusini mashariki mwa Ukraine umethibitisha sera ya
Urusikuwa ilikuwa sahihi lakini amesema Urusi itaheshimu jirani yake
Ukraine kama nchi ndugu.
Akizungumza mjini Basel Uswisi, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema nchi za magharibi hazitaki vita na Urusi.
"Hakuna
anayenufaika na mvutano huu... Si mtindo wetu au matamanio yetu kuona
Urusi ikitengwa kutokana na vitendo vyake yenyewe," amesema Bwana Kerry.
Urusi itaweza kujenga upya imani, amesema, kwa kuondoa misaada kwa waasi wanaotaka kujitenga mashariki mwa.CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment