Hawa ndio punda waliobebeshwa ujumbe na wanaharakati na kuachwa katikati ya Jiji
Kenya ni moja ya nchi
ambazo huwa zinakaa kwenye headlines ya kuwa na story kubwa Afrika
Mashariki, ya leo inahusu punda waliobebeshwa ujumbe maalumu na kuachwa
katikati ya jiji la Nairobi.
Desemba 11 katikati ya jiji la Nairobi
katika moja ya barabara zenye shughuli nyingi ya Moi, lori moja
lilisimama na kushusha punda wapatao 22 walio na maandishi yenye ujumbe “Tumechoka”.
Wanaharakati nchini Kenya
wametajwa kuhusika na hii ambapo pia wamewahi kutumia njia mbalimbali
ili kufikisha ujumbe wao ambapo moja ya waliyowahi kuifanya ni ile ya
kuyabeba majeneza idadi sawa na Wabunge.
Taarifa zinasema kuwa huu mtindo wa
kuwashirikisha wanyama kwenye maandamano ya kudai haki ilianzishwa na
mwanaharakati ambaye pia ni mkurugenzi wa Pawa 254, Boniface Mwangi japo
safari hii haijafahamika sababu ya kuwatumia wanyama hao kufikisha
ujumbe huo.
“Tumechoshwa na uongozi mbaya… ” alisikika mmoja ya wanaharakati huku akiwasukuma punda hao kutoka nje ya Lori.Polisi wanasema wanawasaka wale waliohusika na kitendo hicho.
No comments:
Post a Comment