Iraq yabaini wanajeshi hewa
Uchunguzi
wa idara ya kupambana na vitendo vya rushwa nchini Iraq umebaini kuwepo
kwa wanajeshi hewa 50,000 katika orodha ya malipo ya mishahara.
Askari
hao wajulikanao kama askari mizimu yaani Ghost soldiers hawajawahi
onekana kazini japo kuwa mishahara yao ilionekana kuendelea kulipwa kwa
watu wasiojulikana.
Taarifa
kutoka ofisi ya waziri mkuu wa Iraq ofisi yake imechukua hatua kuhusiana
na tatizo hilo na tayari malipo ya mishahara hiyo ya skari hewa
imekwisha simamishwa.
Vitendo
vya rushwa ndani ya jeshi la Iraq vinatajwa kuchangia kurudisha nyuma
vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiislam IS Kaskazini na Magharibi
mwa taifa hilo.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment