Tanzania yazidi kuporomoka viwango vya kimataifa vya FIFA
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imezidi kushuka katika viwango vya ubora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na sasa imeshuka kwa nafasi moja zaidi na kushika nafasi ya 140.
Orodha hiyo imetolewa jana na Shirikisho
la soka duniani FIFA na imeonyesha kuwa, Tanzania ndiyo nchi inayoshika
nafasi ya chini zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Uganda
inashika nafasi ya 74, huku Kenya ikiwa ya 116.
Algeria ndiyo inayoongoza kwa Afrika kwa kushika nafasi ya 19 ikifuatiwa na Ivory Coast inayoshika nafasi ya 21.
Timu zinazoongoza katika nafasi 10 bora ni; Argentina, Ubelgiji, Ujerumani, Colombia, Brazil, Ureno, Romania, England, Wales na Chile.
No comments:
Post a Comment