Picha za mtoto wa Whitney Houston akiwa kwenye jeneza ni biashara? familia je?..

Bobbi Kristina 
amefariki akiwa na miaka 22 baada ya kuugua muda mrefu kutokana na 
kudondoka bafuni..sababu ikidaiwa ni kuzidiwa na dawa za kulevya 
alizokua akitumia.
August 3 ilikuwa siku ya mazishi yake, 
 baada ya kumalizika familia yake imeamua kuuza picha za marehemu Bobbi 
Kristina akiwa ndani ya jeneza kwa dola 100,000 sawa na zaidi ya 
200,000,000 za Kitanzania.
Uamuzi wa familia yake ni mwendelezo kwani mama yake mzazi marehemu Whitney Houston naye picha zake zilikua zikiuzwa na kuchapishwa na watu maalum kutoka Makumbusho ya Taifa.
Wakati wa kuandaa mazishi yake familia 
ya Houston ilikua makini sana kuhakikisha picha za marehemu mtoto wao 
akiwa ndani ya jeneza hazivuji huku Shangazi yake Bobbi Kristina aitwaye
 Leolah Brown akisimamia kazi hiyo.
Bobbi Kristika amezikwa pembeni ya kaburi la mama yake Whitney Houston August 3 katika makaburi ya Westfield yaliyopo New Jersey, Marekani.



No comments:
Post a Comment