TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, August 7, 2015

Kauli ya Di Maria kuhusu Manchester United bado inawashangaza walio wengi

Kauli ya Angel Di Maria infanya watu wazidi kujiuliza maswali mengi na yasiyo na majibu, muda mchache baada ya kuthibitika kujiunga na klabu ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa Di Maria amesema klabu ya PSG ni kubwa kuliko klabu yake ya zamani ya Manchester United.
angel-di-maria-4-h
Bado haijajulikana au kupatikana kwa majibu halisi ni kitu kipi amekitumia kupima ukubwa wa klabu hizi mbili moja ni ushabiki au mapenzi yake kwa PSG au kaamua tu kuzungumza kwa sababu kahama Man United bado anatuachia maswali mengi yasiyo na majibu ni kigezo kipi katumia kuvitofautisha vilabu hivi.
download
Kama kweli PSG ni kubwa kwa kigezo kipi kama umri wa vilabu hivi ni tofauti Manchester United ni kubwa kwa jumla ya miaka 137 huku PSG ina miaka 44 pekee ni kubwa kwa miaka mitatu dhidi ya mkongwe wa Man United Ryan Giggs na kama kwa mataji PSG ina jumla ya mataji yasiyo zidi 30 huku Man United wakiwa na mataji zaidi ya hamsini huku ni kuudanganya umma.
Di Maria ni mchezaji wa pili wa PSG kusema klabu hiyo ni kubwa kuliko Manchester United baada ya beki wa Kibrazil Thiago Silva kutoa kauli hiyo siku kadhaa nyuma.

No comments:

Post a Comment