Leo nimepita kwenye hili soko la Samaki, takwimu na idadi ya wafanyabiashara hizi hapa
Kazi yangu ni kuhakikisha nakusogezea
kila stori inayonifikia na leo nimepita Feli Dar es Salaam ambapo ni
eneo linalohusika na shughuli za uvuvi wa Samaki.
Inawezekana ukawa ni mpenzi wa chakula
cha Samaki lakini haufahamu kinatoka sehemu gani na ndio sababu kubwa
iliyonifanya nije hapa kwenye hili soko kuu ili nikusogezea kila ambacho
haukifahamu.
Baada ya kufika kwenye soko hilo nimefanikiwa kumpata Mwenyekiti wa
soko Ally Kibwana ambaye ameelezea namna ya uvuvi wa samaki pamoja na
idadi ya wafanya biashara katika eneo hilo.
‘Kwa muda wa kawaida samaki kuwapata
tunapata tani milioni moja kwa siku kutokana na kuingia kwa samaki
sehemu mbalimbali Mafia, Kilwa na wavuvi wetu wa hapa wanaoenda na
kurudi kwa hiyo kutokana na hali ya bahari kubadilika kutokana na tabia
ya nchi kuna upepo mkali ambao umesababisha samaki kidogo kupungua kwa
hiyo hatufiki kile kiwango tunachokihitaji’ – Ally Kibwana
‘Kazi moja ngumu ya Uvuvi kwasababu
mfano uvuvi wa madagaa tunatumia nyavu na kuna uvuvi ambao tunatumia
boti hizi ndogo tunazihitaji ngwanda ni kutupa nyavu kutega ukishatega
halafu watu wanashuka chini kuzisukuma zile nyavu ili kupata samaki
lakini ni moja kati ya kazi ngumu kwasababu bado tuna uvuvi wetu wa
kizamani hatujapata uvuvi wa kisasa kama tulivyoahidiwa na Serikali’ –
Ally Kibwana
‘Wafanyabiashara waliopo hapa feli wanakaribia elfu kumi sasa hivi
walipo sokoni kwasababu tupo katika kata kuna zone namba 1 mpaka namba
8, zone 8 ambayo inashughulika kuvua na kurudisha mali na kuja kuuza
zone namba 1, toilet hapa ziko mbili ambao zinauwezo wa kuingiza mara
moja watu kumi lakini hazitoshi kwasababbu watu ni wengi tathmini ya
mwanzo ilikuwa ni watu elfu 10000 ila kwasasa wamezidi yaani idadi
imeongeza’ – Ally Kibwana.
No comments:
Post a Comment