Burundi: hali ya wasiwasi yatanda Bujumbura
Pierre-Claver
Mbonimpa, mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Burundi, alizuiliwa
jela kwa zaidi ya miezi minne. Hapa ni wakati alipokua Mahakamani
akisubiri kusikilizwa, Julai 4 mwaka 2014.
Na RFI
Mwanaharakati
wa haki za binadamu akiwa pia kiongozi wa shirika linalotetea haki za
binadamu na za wafungwa APRODH, Pierre-Claver Mbonimpa ameponea kuuawa
baada ya kujeruhiwa kwa risasi alizovyatuliwa na mtu aliyekuwa kwenye
pikipiki katika kata ya Kanga wilayani Kinama, Kaskazini mwa jiji la
Bujumbura.
Hali ya wasiwasi imetanda katika mji wa Bujumbura na wakaazi wa mji huo wameingiliwa na hofu baada ya kusikia tukio hilo.
Uvumi wa
kuuawa kwa Pierre-Claver Mbonimpa ulianza kuzagaa tangu Jumapili Agost 2
nchini Burundi. Lakini Jumatatu mchana wiki hii, mwanaharakati huyo
amekanusha taarifa hiyo.
Saa
zisiozidi nne baadae, yaani saa 12 na robo, mtu aliye kuwa kwenye
pikipiki amemfyatulia risasi Pierre-Claver Mbonimpa wakati alipokua
akirudi nyubani katika kata ya Carama wilayani Kinama, Kaskazini mwa
jiji la Bujumbura.(P.T)
Pacifique
Nininahazwe, mmoja kati ya wanaharakati wa mashirika ya kiraia akiwa
pia kiongozi wa muungano wa mashirika ya kiraia FOCODE, yanayopinga
muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza, ametoa wito wa kuzidisha ulinza
katika hospitali ya Polyclinique Centrale de Bujumbura anakolazwa
Pierre-Claver Mbonimpa, akisema anahofu huenda mwanaharakati huyo
akamaliziwa maisha.
Balozi wa
Marekani amewasili katika hospitali anakolazwa Pierre-Claver Mbonimpa,
huku akielezea masikitiko yake kuona mauaji yamekua sugu nchini Burundi,
hususan katika mji mkuu wa Bujumbura.
Hayo
yanajiri wakati hali ya wasiwasi imetanda mjini Bujumbura na katika
vitongoji vyake. Hali hii inatokea wakati katika hotuba yake Jumapili
jioni baada ya kifo cha mkuu wa zamani wa Idara ya Ujasusi, jenerali
Adolphe Nshimirimana mapema jumapili asubuhi, rais wa Burundi Pierre
Nkurunziza aliwatolea wito raia kuwa watulivu na kujizuia na chochote
kile ambacho kinaweza kuchochea chuki na machafuko.
Hata
hivyo milio ya risasi imeendelea kusikika Jumatatu jioni wiki hii katika
wilaya ziliyokuwa za waandamanaji hususan Nyakabiga, Cibitoke na Bwiza.
Mpaka sasa haijajulikana hasara iliotokea.
Jumapili
asubuhi afisa mwengine wa Idara ya Ujasusi wilayani Musaga, aliuawa
nyumbani kwake na watu wasiojulikana. Mauaji yamekithiri nchini Burundi,
ambapo mauaji yamekua yakishuhudiwa kila kukicha
No comments:
Post a Comment