TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, August 4, 2015

Hii ni good news kwa mashabiki wa kike wa Manchester United (Pichaz)

 

446407-e9b0defc-395f-11e5-b9fd-ad0b337aa4fa
Siku kadhaa zimepita toka klabu ya Manchester United ya Uingereza itangaze jezi zake mpya na kampuni itakayokuwa inatengeneza jezi hizo, August 3 nimekutana na story nyingine tena kwa ajili ya mashabiki wa kike wanaoipenda Mancheater United… Zamani tulizoea kuona mashabiki wa kike wa Manchester United Tanzania na hata Uingereza wakivaa jezi za kiume wanapoenda uwanjani na sehemu zingine za kutazamia mechi kwa njia ya TV.
shirt-comp
Manchester United hawakuishia tu kutengeneza jezi za kiume zitakazotumiwa na wachezaji na mashabiki wa kiume, kampuni ya ADIDAS ambayo ndio yenye mkataba na Man United katika kipindi cha miaka 13 ijayo, imetoa jezi kwa ajili ya mashabiki wa kike.
f17786fa-2ebf-4764-ad56-105a96d9775c_16x9_600x338
Kushoto ni jezi ya Kike na upande wa kulia ni jezi ya kiume
Man United wameingia mkataba wa miaka 13 wenye thamani ya pound milioni 750 na kampuni ya vifaa vya michezo ya Kijerumani ADIDAS baada ya mkataba wa miaka 10 na kampuni ya Nike kumalizika.
446407-e9b0defc-395f-11e5-b9fd-ad0b337aa4fa

No comments:

Post a Comment