Mabadiliko ya tabia ya nchi kupata Dawa?

Rais wa Marekani, Barack Obama
Rais wa Marekani, Barack Obama amezindua kile alichokiita hatua muhimu zaidi ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Amesema kizazi hiki ni cha mwisho chenye kushughulikia suala hilo na kwamba imelazimu Marekani kuchukua hatua.
Obama 
amesisitiza hatua kali kuchukuliwa haraka, kupunguza gesi ya ukaa 
inayotoka katika viwanda nchini Marekani, theluthi moja, ifikiapo mwaka 
2030.
Wachambuzi
 wa mambo wanasema mpango huo unatazamwa kama changamoto kwa nchi 
nyingine zikielekea kabla ya mkutano mkuu utakaofanyika jijini Paris.
Umoja wa 
Mataifa umepokea vyema mpango wa Marekani pia Umoja wa Ulaya huku 
ukipingwa vikali na wapinzani kutoka chama cha Republican.BBC
No comments:
Post a Comment