Hii ni sababu iliyomtoa Rafael da Silva Man United, Van Gaal anahusika
Ikiwa zimepita siku kadhaa toka aliyekuwa beki wa pembeni wa klabu ya Manchester United ya Uingereza Rafael da Silva aondoke klabuni hapo na kutimkia katika klabu ya Olympique Lyon inayoshiriki Ligi Kuu Ufaransa kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kufikia pound milioni 2.5.
August 12 amefunguka na kusema kuwa kilichomtoa hapo ni kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal
 kutokuwa ana muhitaji na kukiri kuwa kocha huyo hakuwa hakimpenda hivyo
 hiyo ni miongoni mwa sababu zilizo mpelekea kuondoka klabuni hapo.
Rafael alizungumza hayo baada ya kuulizwa kuhusu kuondoka kwake ni kweli Van Gaal hawapendi wachezaji wa kibrazil, Rafael anakiri kusikia hiyo story ya Van Gaal
 kutopenda wachezaji wa Kibrazil ila hawezi thibitisha kuwa ndio 
hawapendi ila anachojua hata yeye hakuwa anapendwa na kocha huyo.
“Nilisikia
 hii story ya kuwa hawapendi wachezaji wa Kibrazil lakini siwezi sema 
hivyo kwani sina uhakika, najua alikuwa hanipendi labda sababu ya mimi 
kuwa Mbrazil hilo sijui. Nilicheza msimu mzima wa 2012-2013 nikiwa chini
 ya Ferguson nilicheza kila mechi ulikuwa msimu bora nikiwa Man United 
kiasi cha kutwaa Ubingwa”>>>Rafael
Beki huyo mwenye umri wa miaka 25 alicheza kwa miaka saba katika klabu ya Manchester United kabla ya kuondoka wiki iliyopita na kujiunga na klabu ya Olympique Lyon ya Ufaransa, wakati huo Man United  ilikuwa ikinolewa na kocha Sir Alex Ferguson.



No comments:
Post a Comment