WACHEZAJI RAJA CASABLANCA WAGOMBEA VIATU VYA RONALDINHO
Wachezaji wa Casablanca wakisaka viatu vya Ronaldinho (HM)


MARA tu baada ya kutolewa katika Klabu
 Bingwa ya Dunia a FIFA, wazi Ronaldinho alitaka kurejea chumba cha 
kubadilishia nguo cha Atletico Mineiro kujiliwaza.
Lakini alilazimika kubaki uwanjani 
baada ya kuvamiwa na wachezaji wa Raja Casablanca, waliomsalimia na 
kumuomba viatu vyake vya Nike!
Timu hiyo Morocco iliendeleza wimbi 
lake la ushindi nyumbani kwa ushindi wa mabao 3-1, wakimtoa nishai 
Mbrazil huyo ambaye alifunga bao zuri la mpira wa adhabu- katika 
jitihada zake za kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza tangu alipofika 
fainali akiwa na Barcelona mwaka 2006. Chanzo: binzubeiry

No comments:
Post a Comment