MAAFA -UKAME
Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa -
Ofisi ya Waziri Mkuu Lut Jen (Mst) Sylivester Rioba akieleza umuhimu wa
Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo Wa Kupunguza Athari Za Maafa Kwa Mikoa
Iliyoathirika Zaidi Na Ukame wakati wa Uzinduzi wa Mradi huo kwa Wilaya
ya Kishapu, Shinyanga jana, katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya
Kishapu (watatu kushoto) Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu Bw. Octavian
Mangosongo. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu).
Vijana Kutumika Katika Kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo Wa Kupunguza Athari Za Maafa Ya Ukame.
Na. Mwandishi Maalum
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Maafa imesema itawatumia vijana walioko shuleni na nje ya shule katika Mradi wa kuzijengea uwezo jamii wa kuzuia, kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame. Kauli mbiu ya Mradi huo ni " Athari za Ukame Zinapunguzika, Jamii ikielimishwa."
Akiongea wakati wa Uzinduzi wa Mradi huo jana wilayani Kishapu, Mkurugenzi Wa Idara Ya Uratibu Wa Maafa, Ofisi Ya Waziri Mkuu, Lut Jen (Mst) Sylivester Rioba alisema lengo la kujumuisha vijana walioko shuleni na nje ya shule, ni kuwajengea utamaduni wa kutambua viashiria na vihatarishi vinavyoweza kusababisha maafa ili waweze kukabiliana na maafa yanapotokea na hatimaye kuwaanzishia miradi midogo midogo ya ufugaji na Kilimo kwa ajili ya kipato na kujikimu na maisha.(P.T)

"Kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi
yameleta athari nyingi ikiwemo ukame, kupitia mradi huu ulioanza
kutekelezwa kwa majaribio katika Wilaya ya Same kwa Mkoa wa Kilimanjaro
na Wilaya ya Kishapu kwa Mkoa wa Shinyanga vijana na akina mama
wataelimishwa juu ya upandaji wa miti na kilimo cha mazao yanayohimili
ukame hususan mihogo na viazi vitamu." Alisema Rioba
Rioba alifafanua kuwa katika kuijengea jamiii uwezo wa kukabiliana na kupunguza vihatarishi vinavyoweza kusababisha maafa ya ukame mradi utaainisha na kutoa mafunzo kwa wadau kuhusu matumizi ya mbegu na pembejeo za kilimo, mifugo na misitu. Pia mafunzo kwa wataalam kuhusu matumizi ya vifaa vya kukusanyia takwimu na mawasiliano yatatolewa pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu na mifugo utaboreshwa.

No comments:
Post a Comment