SUDAN KUSINI YATIBUA JARIBIO LA MAPINDUZI
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir,
anasema vikosi vyake vimefanikiwa kutibua jaribio la mapinduzi, baada ya
usiku mzima wa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.
Bw. Kiir, anayetoka katika kabila
kubwa zaidi la wa Dinka amewatupia lawama wanajeshi wanaomtii aliyekuwa
makamu wake Riek Machar, anayetoka katika kabila dogo la Nuer.
Aidha Kiir ametangaza amri ya kutotembea usiku mjini Juba na kusema serikali sasa inaudhibiti mji huo.
Makundi hasimu ya wanajeshi walipigana
vikali kwa saa kadhaa na kuna ripoti za kuwepo majeruhi maelfu
wakiripotiwa kukimbilia usalama wao.
Milio ya risasi sasa inaripotiwa
kupungua. Kumekuwa na hali tete ya kisiasa nchini Sudan Kusini tangu
mwezi Julai wakati Rais Kiir alipovunja na kuwafuta kazi mawaziri wote
katika baraza lake akiwemo Makamu wa Rais Bw.Machar.(P.T)
No comments:
Post a Comment