JESHI LA CONGO DR LAREJESHA HALI YA UTULIVU KINSHASA

Jeshi la demokrasia ya Congo limesema 
kuwa limefanikiwa kuzima shambulio lililolenga uwanja wa ndege na kituo 
cha taifa cha Radio na Televisheni linalodaiwa kutekelezwa kundi 
lisilofahamika la kigaidi.
Waziri wa habari nchini humo Lambert 
Mende kwa sasa hali imedhibitiwa ambapo wamefanikiwa kuwaua watu 40 
miongoni mwa waliokuwa wakiendesha mashambulizi hayo.
Watu hao waliokuwa na silaha 16 kati 
yao wameuawa katika mapambano na polisi uwanja wa ndege,16 wengine 
katika eneo la jeshi na nane wao waliuawa katika ofisi za Radio ya 
Taifa.
Amesema kuwa kulikuwa na mtukio mengine mawili ya mashambulizi katika maeneo ya uwanja wa ndege na kambi ya jeshi.
Kwa mjibu wa waziri Mende watu hao 
waliokuwa wakiendesha mashambulizi hayo katika televisheni ya taifa na 
makao makuu ya radio ya taifa walikuwa na silaha zikiwemo bunduki,visu 
lakini walidhibitiwa kabla ya kusababisha madhara .
Mashambulizi haya yametokea wakati rais Joseph Kabila akiwa ziarani katika jimbo la Katanga nchini humo.
Ubalozi wa Marekani umetoa tahadhali kwa raia wake kutofanya safari za ndani ya mji wa Kinsasa hadi hali itakapodhibitiwa Zaidi.(P.T)
No comments:
Post a Comment